Wilson Abubakar Radido, anayefahamika kwa jina la kisanii Willy Paul, alizaliwa Septemba 1993 mjini Nairobi, Kenya. Ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwanzilishi wa Saldido International Entertainment, anayejulikana kwa uwezo wake wa kubadilika kimuziki. Amefanikiwa kutoa nyimbo zilizopendwa kama “Sitolia,” “You Never Know,” “Tam Tam,” “I Do,” “Njiwa,” na “Mmmh,” huku akishirikiana na wasanii wakubwa akiwemo Nandy, Rayvanny, Yemi Alade, Alaine, na Khaligraph Jones.
RELATED: Willy Paul – Ngunga
Tarehe 09 Januari 2026, Willy Paul anarejea na wimbo mpya wenye nishati kubwa uitwao “Party This Year (Double Double).” Wimbo huu ni wa shangwe na burudani, ukiwahamasisha mashabiki kufurahia maisha na mafanikio. Kwa midundo ya kuchezeka na chorus inayonata, “Party This Year” ni wimbo unaofaa kwa sherehe, vilabu na matukio makubwa, ukiendelea kuthibitisha ubora wa Willy Paul katika muziki wa Afrika Mashariki. Wimbo huu unapatikana exclusive kwenye Side Makini Blog.
AUIDO | Willy Paul – Party This Year (Double Double) | Download Mp3
Explore More songs from Diamond Platnumz:

Leave a Comment