Audio

Diamond Platnumz – Moyo (Official Lyric Audio)

LYRICS Diamond Platnumz – Moyo (Official Lyrics Audio) Side Makini Blog
LYRICS Diamond Platnumz – Moyo (Official Lyrics Audio) Side Makini Blog

Renowned Tanzanian artist Diamond Platnumz drops yet another hit titled “Moyo”, a song about patience and resilience in tough times. Released on February 13, 2025, this masterpiece, produced by MrLG and mixed by Lizer Classic, brings out the emotional depth that Diamond is known for.

RELATED: Diamond Platnumz – Nitafanyaje

The Official Lyric Audio, available on YouTube, lets fans vibe along with the heartfelt lyrics.

Verse 1

Pole pole pole,
Pole pole,
Moyo wangu,
Masikini pole,
Pole mtima wangu.

Haikuwa dhamira,
Haikuwa kusudi langu,
Haikuwa dhumuni waala,
Haikuwa malengo yangu.

Ila tuseme,
Labda moyo,
Pengine sio,
Ridhiki.

Maana,
Nimejitahidi sana,
Malengo hayafiki.
Kama kuswali,
Naswali sana,
Mpaka sunna za usiku.

Kazi nimetafuta sana,
Ila siambulii kitu.
Sitaki kukufuru Mungu,
Sababu najua ni mapito.
Japo inakatisha tamaa,
Ila siku yangu ipo.

Chorus

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

Moyo wangu, moyo,
Usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

(Instrumental)

Verse 2

Penzi maua,
Pesa mbolea.
Hata shemeji yako,
Ana mengi ila,
Hawezi ongea.

Moyo,
Najitahidi jiepusha vya watu,
Ni majaribu aah,
Japo nna shida,
Ila naepuka tamaa.

Moyo,
Nlitamani siku moja,
Na mimi nimjengee mama,
Ila ndo vile tu umasikini,
Mipango inakwama.

Hua naumia,
Watoto shuleni,
Wakifukuzwa ada.
Najiona mjinga,
Yani sio bora baba.

Sitaki kukufuru Mungu,
Najua ni mapito.
Maana riziki mafungu,
Nami langu siku lipo.

Chorus

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

(Instrumental fade out…)

Watch & Sing Along Below:

Enjoy the vibe and feel the message!

Explore More songs from Diamond Platnumz:

Leave a Comment