
Saidi Ramadhani Ally alizaliwa Singida Aprili 22 akiwa ni mtoto wa mwisho kwenye famili ya watoto 7 ya Ally ambae ni mnyiramba wa kiomboi Iramba, ni mkulima na mfugaji na Mama Mbogo ni mjasiriamali.
Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Saidi, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana, shule ya awali alianza mnamo 2003,
Na darasa la kwanza alianza mwaka 2004 hivyo alifanya vizuri sana katika shule ya msingi, hata hivyo alisoma shule mbili tofauti, ikiwa ni pamoja na shule ya msingi Nsonga iliyopo katika Wilaya ya Iramba, na alipofika darasa la tatu mama yake alihama alipokuwa akiishi na kulazimu kumhamisha shule na akenda kuendelea na masomo ya shule ya msingi Mwanduigembe na huko ndiko iliko familia yao.
Kimsingi katika maisha kuna kuanguka na kufeli kiufupi kuna misukosuko mingi sana, ndiyo hivyo ilivyokuwa kwa Saidi Ramadhani Ally na familia yake kiujumla kulitokea ugomvi na tafaruki nyingi ikabidi mama mzazi wa Saidi Ramadhani, kuondoka nyumbani na kumchukua Saidi akiwa bado yupo katika elimu ya msingi, aliongozana na ndugu yake aliyekuwa kaka yake aliyejulikana kwa jina la Hamissi, huyu Hamissi kwa mwaka huo wa 2009 yeye tayari alisha hitimu elimu ya msingi lakini hakubahatika kuendelea na shule/kufaulu mitihani ya darasa la saba ya kumuwezesha kwenda sekondari.
na hatimae Saidi safari yake ya shule iliishia hapo na hakuweza tena kuendelea na masomo ama shule kutokana na maisha na mazingira waliyokutana nayo huko waliko elekea.
Waliondoka na kwenda mipakani mwa mkoa wa Singida, kiufupi waliingia mkoa wa Tabora katika wilaya ya Igunga, kijiji cha Mwanzuki, huko walifika katika familia ya Mzee Benard aliyekuwa ni msukuma aliye elimika, hapo waliishi kama wafanyakazi kiujumla na maisha yao katika familia ya Mzee Benard yalidumu kwa mwaka mmoja na nusu.
Hivyo walirudi tena mkoani Singida na safari hii walifikia katika kata ya Kaselya huko ndiko kulikuwa na chimbuko la ukoo wao maana baadhi ya ndugu walikuwepo huko, hivyo maisha yao yalianza upya 2011, walianza kujishughulisha na kilimo huku wakiwa na eneo dogo sana, maisha yaliendelea kama kawaida
Mwaka mmoja baadaye Saidi alipata fursa ya kazi ambayo alipewa na ndugu yake Hamissi, hivyo ilibidi aende zake wilaya ya Iguguno kwa ajili ya kazi na kumuacha Mama yao akiwa mwenyewe tu lakini haikuwa shida sana kwa sababu alikuwa na familia ya baadhi ya ndugu wa ukoo wao akiwemo mdogo wake aliyetambulika kwa jina la Mama Pili/Mama Ally (Nahali).
Huko Iguguno alipata fursa ya kazi ya Kulisha mifugo ikiwemo Ng’ombe na Mbuzi, Kondoo, na mshahara ulikuwa ni mia tano kwa siku, hivyo kwa mwezi ni elfu kumi na tano! hakudumu sana katika kazi hiyo kutokana na ugumu wa kazi ukilinganisha na mshahara wake.
Mwaka 2013, mama mzazi wa Saidi alishauriwa na waliokuwa watoto wake waliotambuliwa kwa majina kati ya Gress na Ramadhani Mbogo, arudi nyumbani katika familia na haikuwa ngumu sana mama alirudi katika familia, mwaka huo huo naye Saidi na Hamissi na wao walirudi tena nyumbani huko ni Mwanduigembe,
waliendelea na maisha yao mwaka mmoja huo Saidi alitumia nafasi hiyo katika kilimo, kama bahati 2014, alipata fursa ya kazi Jijini Dar es salaam, fursa hiyo alipewa na aliyekuwa dada yake mwenye jina Tatu Gyunda, aliamua kuondoka nyumbani na kwenda Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kazi alifikia Tegeta na alianza kufanya kazi ya Duka, la vyakula hususani vinywaji Duka hilo lilikuwa la Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Mzee Mbaga, na duka lilikuwa na Jina la “Mbaga Shop”
Unaambiwa malipo ni hapa hapa duniani, baada ya saidi kuwa Dar es salaam, alimpa fursa ndugu yake aliyekuwa amempa shavu mara ya kwanza huko Singida katika kazi ya Kulisha mifugo! alimwambia kwamba kuna kazi huku Dar es salaam kama upo tayari njoo ufanye naye Hamissi alikubali na kufanya hivyo!
Saidi amewahi kujihusisha na muziki kama msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, katika muziki akitumia jina la Mkali Swaxc, 2016 aliungana na wasanii wengine ambao walikuwa wakifanya muziki lakini hawakuwa Wasanii maarufu Wasanii hao wakitambulika kwa majina yafuatayo, Han Boy Classic, Unique Flavour, Wamtani B, pamoja na mwanadada mrembo aliyekuwa ni mke/mpenzi wa Han Boy Classic, mwadada huyo kwa jina*** waliungana kwa pamoja na kuunda kundi/band iliyo kwenda kwa jina la Swaxc Band, lakini haikudumu kutokana na maisha yao kuwa duni.
Maisha yalienda hatimaye 2016, alipata wazo la kuja na blog kwa mara ya kwanza alifungua blog iliyokuwa na kiunga cha www.sidemakini.blogspot.com baada ya miezi kadhaa mbele alinunua kikoa (domain) na kuhama kutoka blogger kwenda katika WordPress Blog, iliyo kuwa na kiunga www.sidemakini.com ambayo kwa sasa hupatikana katika kuunga cha www.sidemakini.co.tz
Tovuti ya Side Makini Blog, inajihusisha na upakiaji wa muziki Tanzania na Afrika kiujumla pia huweka makala mbalimbali kutoka katika tovuti mbalimbali kwa kuzingatia hatimiliki.
Saidi alianza kutambulika kama Side Makini Entertainer, baada ya kuhusika ku hushughulisha na ukuzaji wa muziki Tanzania, na amesaidia zaidi ya wasanii 10 waliopata mafanikio na walidai kwamba wasitajwe katika uzi huu, Side Makini Entertainer, alianzisha taasisi yake iliyokuwa ikisapoti wasanii tofauti tofauti kulingana na mahitaji halisi ya msanii
Kumbuka kwamba habari hii sii kamili kwa asilimia mia kutokana na ukubwa wa Side Makini Entertainer hivyo ikihitaji kujua zaidi unashauriwa kuwasilisha naye kwa mawasiliano yafuatayo
Email sidemakini@gmail.com
Call 0783235234
Asante kwa mda wako Side Makini jina Kamili ni Saidi Ramadhani Ally ni blogger kutoka Tanzania amezaliwa Aprili 22