Home Makini Music Playlist | Killy – The Best of Killy (All Songs) | Mp3...

Playlist | Killy – The Best of Killy (All Songs) | Mp3 Download Audio

Ally maarufu kama Killy ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania alianza safari yake ya muziki mnamo November 22, 2014 akiwa na wimbo uitwao USIWAZE uliofanyika katika studio za AM RECORDS Chini ya producer Maneck

BONYEZA HAPA KUPATA NYIMBO ZOTE ZA KILLY

2015 aliachia wimbo uitwao RUDI pamoja na video yake iliyo ongozwa na director nisher vilevile audio ilifanyika katika studio za AM RECORDS Chini ya producer Maneck

CLICK HERE TO FIND ALL KILLY SONGS

Hakuwa ni msanii lelemama 2016 aliachia wimbo mwingine uitwao NIKWAMBIE pamoja na video iliyoongozwa na ADAM JUMA  huku Producer akiwa ni MOCCO GENIUS chini ya Label ya ALJAZEERAH MUSIC GROUP pia akiwa anasimamiwa na  Papaa Misifa aliyekuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa na nguvu kubwa ya kukuza muziki.

Kama ilivyo kawaida ya maisha kuna kupanda na kushusha hivyo hivyo ilivyo kuwa kwa KILLY baada ya project na ALJAZEERAH MUSIC GROUP inaonekana hawakuweza kuendelea kufanya kazi pamoja hivyo alikaa kimya takribani miaka mitatu.

Baadaye tena alipata nafasi ya Kusainiwa na Kings Music record label iliyo chini ya Alikiba  akiwa Kings Music alitoa vibao vyake viwili GUBU Aliyo shirikiana na Boss wake Alikiba pia Januari 16/2020 aliichaia kazi mpya iliyokwenda kwa jina la AMENIKAA akiwa ameshirikiana na Nyanda pamoja na Singah huku Producer wakiwa ni S2kizzy na Mocco Genius

Baada ya hapo aliondoka kwa Alikiba na kuaa kimya kwa muda mfupi baadaye akatoa taarifa kuwa yupo katika uongozi mpya amabao ni Konde Gang Worldwide Music Label inayoongozwa na Msanii Harmonize.

(Visited 4,131 times, 3 visits today)