Home Makala Kutumia Simu Chooni Tabia Ya Zaidi Wamiliki 7 Katika 10 Wa Simu...

Kutumia Simu Chooni Tabia Ya Zaidi Wamiliki 7 Katika 10 Wa Simu Janja

Tabia ya kutumia simu chooni imesambaa kwa kasi kubwa kuliko kawaida kwa wamiliki wa simu janja. Tafiti kadhaa zilizofanyika nchini Marekani zinaonesha ni kati ya watu 7 au ata zaidi katika watu kumi wanafanya jambo hilo mara kwa mara.

Tafiti zinaonesha kutumia simu chooni kuna madhara mengi linapokuja suala la afya yako. Tafiti iliyofanywa na kampuni ya utengenezaji display za LED zinazokuja na dawa za kuua vijidudu kama bakteria, ya Vital Vio, ilionesha asilimia 88 ya watumiaji simu janja wanazitumia wakiwa chooni pia, na asilimia 44 huwa na tabia ya kuweka simu mdomoni mara kwa mara.

Hatari ya kwanza: Vijidudu kutoka uchafu wa chooni

Kuna vijidudu/bakteria wa aina mbalimbali wanaotokana na uchafu utokanao na vinyesi. Na hivi vinakuwa ni vidogo na si mara zote uchafu huu unaonekana kila sehemu, hivyo sehemu inayoonekana safi sana kwako ili kuweka simu yako ukiwa chooni inaweza kufikiwa na bakteria hawa.

 

kutumia simu chooni

Kutokana na kujikuta katika maeneo mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na chooni, simu janja zinabeba bakteria wa aina mbalimbali

Tafiti ya mwaka 2018 ya nchini Uingereza ilionesha simu janja za watumiaji wengi ni chafu kuliko ata vyoo vingi vya nchini humo – uchafu huu ni kwa wingi wa aina za bakteria wanaopatiakana kwenye simu hizo. – Insurance2go UK

Hatari ya pili: Magonjwa yanayosababishwa na kukaa chooni muda mrefu

Kwa kawaida bila mtu kuingia na simu chooni wakati wa aja kubwa hawezi kuchukua muda mrefu sana chooni, tafiti zinaonesha mtu atakuwa ashatoka ndani ya dakika 10 – ila akiingia na simu basi anaweza jikuta yupo chooni kwa dakika 10 hadi 30. Madaktari wanasema mtu akiwa na wastani wa kukaa muda mrefu chooni – zaidi ya dakika 15 inaweza sababisha matatizo ya mfumo wa haja kubwa kama vile hali ya kufunga choo ‘constipation’.

simu chooni

Kubali kupumzisha utumiaji wa simu ukiwa chooni

Vipi je wewe pia huwa unatumia simu yako ukiwa chooni? Tunakushauri uwe unachukulia muda huo kama kipindi cha mapumziko dhidi ya utumiaji simu – unaweza, itakuwa inakusubiri ukimaliza.

(Visited 2 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here