Home Makini Buzz Tuzo za MTV za muziki wa Afrika 2020: Orodha kamili yawaliochaguliwa

Tuzo za MTV za muziki wa Afrika 2020: Orodha kamili yawaliochaguliwa

Orodha ya wanamuziki wenye vipaji waliochaguliwa kwa ajili ya kupata tuzo za muziki wa Afrika la MTV Africa Music Awards (MAMAs), imetangazwa huku majina maarufu na mapya yakijitokeza tena kwenye orodha hiyo.

Tukio la kutoa tuzo hizo za mwaka 2021 litafanyika mjini Kampala Uganda tarehe 21 Februari 2020 kwa njia ya mtandao kutokana na janga la virusi vya corona.

Tiwa Savage mwanamuziki wa Nigeria ameng'ara tena kwa tuzo zaidi ya moja
Maelezo ya picha,Tiwa Savage mwanamuziki wa Nigeria ameng’ara tena kwa tuzo zaidi ya moja

Wanamuziki wa Afrika wenye vipaji waliochaguliwa ni pamoja na Burna Boy, Busiswa, Davido, Diamond Platnumz, Innoss’B, Kabza De Small, John Blaq, Master KG, Suspect 95, Sheebah, Soraia Ramos, Tiwa Savage, Yemi Alade and WizKid – ambao kila mmoja amechaguliwa kwa tuzo mbili.

Burna Boy
Maelezo ya picha,katika ukurasa wake wa Twitter mwaka huu Burna Boy alisema yeye ndiye bora baada ya Fela Anikulapo Kuti

Ni nani walioongoza?

Kikundi cha muziki cha São Tomé and Príncipe -Calema waliongoza kwa kuteuliwa tuzo tatu za Msanii wa mwaka, Kikundi bora zaidi cha mwaka , na Kikundi bora kilichoigiza mtindo wa muziki wa Kireno wa Lusophone.

Wasanii waliochaguliwa kwa tuzo za MAMA 52 kutoka nchi 15 walitangazwa katika kipindi cha muziki cha MTV Base Jumatano jioni katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kilitangazwa katika MTV Base.

Zuchu ni miongoni mwa wanamuziki waliopata tuzu kwa kupata mafanikio ya kimuziki
Maelezo ya picha,Zuchu ni miongoni mwa wanamuziki waliopata tuzo kwa kupata mafanikio ya kimuziki

Ifuatayo ni orodha kamili ya wanamuziki walioteliwa kwa ajili ya Tuzo za MAMA 2021 Awards na makundi yao walivyoshinda:

Mwanamuziki bora wa kike:

Simi (Nigeria)

Sheebah (Uganda)

Sho Madjozi (South Africa)

Busiswa (South Africa)

Yemi Alade (Nigeria)

Soraia Ramos (Cape Verde)

Tiwa Savage (Nigeria)

Mwanamuziki bora wa kiume:

Burna Boy (Nigeria)

Innoss’B (Democratic Republic of Congo)

Kabza De Small (South Africa)

Harmonize (Tanzania)

Fireboy DML (Nigeria)

Master KG (South Africa)

Rema (Nigeria)

Kikundi bora cha muziki

Blaq Diamond (South Africa)

Sauti Sol (Kenya)

Kabza De Small / DJ Maphorisa (South Africa)

Calema (São Tomé and Príncipe)

Ethic (Kenya)

Rostam (Tanzania)

Msanii wa mwaka:

Burna Boy (Nigeria)

Calema (São Tomé and Príncipe)

Diamond Platnumz (Tanzania)

Master KG (South Africa)

Davido (Nigeria)

Tiwa Savage (Nigeria)

Wizkid (Nigeria)

Msanii aliyepata mafanikio :

Elaine (South Africa)

Tems (Nigeria)

Omah Lay (Nigeria)

Zuchu (Tanzania)

John Blaq (Uganda)

Sha Sha (Zimbabwe)

Focalistic (South Africa)

Mwanamuziki bora wa Hip Hop

Nasty C (South Africa)

Suspect 95 (Cote d’Ivoire)

Khaligraph Jones (Kenya)

Kwesi Arthur (Ghana)

NGA (Angola)

OMG (Senegal)

Wasanii bora wa muziki wa Uganda

Sheebah

Bebe Cool

John Blaq

Vinka

Daddy Andre

Spice Diana

Wasanii bora wa muziki wa Lusophone

Calema (São Tomé and Príncipe)

Preto Show (Angola)

Anna Joyce (Angola)

Mr Bow (Mozambique)

Nelson Freitas (Cape Verde)

Soraia Ramos (Cape Verde)

Wasanii bora wa muziki wa kifaransa

Innoss’B (Democratic Republic of Congo)

Suspect 95 (Cote d’Ivoire)

Dip Doundou Guiss (Senegal)

Stanley Enow (Cameroon)

Fally Ipupa (Democratic Republic of Congo)

Gaz Mawete (Democratic Republic of Congo)

Wasanii bora wa muziki wakati wa Lockdown

Diamond Platnumz (Tanzania) – Africa Day Benefit Concert

Black Motion (South Africa) – Red Bull Rendezvous

Niniola ft Busiswa (Nigeria / SA) – Africa Day Benefit Concert

Singuila (Congo) – DCDR Series

AKA (South Africa) – AKA TV

Yemi Alade (Nigeria) – Poverty (live session)

(Visited 9 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here