Home Makini Newz Diego Maradona:Picha ya Maradona huenda ikachapishwa kwenye pesa ya Argentina

Diego Maradona:Picha ya Maradona huenda ikachapishwa kwenye pesa ya Argentina

Siku ya Jumatatu Seneta Norma Durango aliwasilisha muswada bungeni ili kumfanya kiungo huyo, ambaye alifariki wiki mbili zilizopita akiwa na umri wa miaka 60, kuwa kwenye noti ya 1,000 sawa na dola ($ 12, £ 9), noti ya juu zaidi.

Noti hiyo itakuwa na uso wa Maradona upande mmoja na picha ya moja ya mabao yake maarufu, hususan dhidi ya England katika robo fainali ya 1986, kwa upande mwingine, alisema.

Seneta huyo pia alipendekeza kuweka picha yake kwenye mihuri ya kumbukumbu.

“Wazo sio tu kumtambua mtu huyu muhimu zaidi, lakini pia kufikiria suala la uchumi,” Bi Durango alisema.

“Tunahisi watalii wanapokuja hapa watataka kumchukua ‘Maradona’ na kwenda naye.

” Alisema seneta huyoPicha ya marehemu nyota wa Argentina Diego Maradona, aliyeiongoza nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1986, inaweza kuwa ndio uso wa noti yenye thamani kubwa zaidi nchini Argentina hivi karibuni.

M

Mchezaji nyota wa zamani wa kandanda Diego Maradona alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 60.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Argentina awali mwezi uliopita alifanyiwa upasuaji wa ubongo ambao madaktari walimwambia ulifaulu.

Baada ya upasuaji huo, ilitangazwa kuwa Maradona angeanza matibabu ya uraibu wa pombe.

Maradona ni moja ya wachezaji bora zaidi wa kandanda kuwahi kutokea.

Mwaka 1986 akiwa nahodha wa Argentina, aliliongoza Taifa lake kushinda Kombe la Dunia nchini Mexico huku akionesha uwezo binafsi mkubwa katika ushindi huo.

Alizichezea klabu za Barcelona ya Uhispania na Napoli ya Italia.

Akiwa na Napoli alinyakua ubingwa wa ligi ya Serie A kwa misimu miwili.

Maradona aliifungia Argentina magoli 34 katika michezo 91, akishiriki michuano minne ya Kombe la Dunia.

madona

Aliliongoza Taifa lake katika fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1990 nchini Italia, ambapo walifungwa na Ujerumani Magharibi.

Alikuwa tena nahodha wa taifa lake katika mashindano ya 1994 nchini Marekani lakini alirudishwa nyumbani baada ya kubainika alitumia dawa za kuongeza nguvu.

Katika miaka yake ya mwisho ya uchezaji aligubikwa na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli pamoja na dawa za kulevya.

Maradona alitaabika na matumizi na uraibu wa dawa za kulevya aina ya cocaine na alifungiwa kucheza mpira kwa miezi 15 baada ya kubainika kuwa alikuwa akitumia dawa hizo mwaka 1991.

Alistaafu kusakata kandanda la kulipwa mwaka 1997 katika siku ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwake, akiwa na klabu maarufu nchini Argentina ya Boca Juniors.

Argentina’s A-team: Maradona, then manager of the national side, passes on his wisdom to forward Lionel Messi at the 2010 World Cup but they are beaten 4-0 by Germany in the quarter-finals

Maradona alichaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Argentina mwaka 2008 na akaachana na kibarua hicho baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambapo Argentina ilitolewa na Ujerumani katika hatua ya robo fainali.

Baada ya hapo akaenda kuvinoa vilabu kadhaa katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu na kisha Mexico.

Mpaka umauti unamfika alikuwa na timu ya Gimnasia y Esgrima inayoshiriki ligi kuu ya Argentina.

(Visited 3 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here