Home Makini Newz Sudan: Shule ya kidini inayowafunga wavulana minyororo yafuchuliwa

Sudan: Shule ya kidini inayowafunga wavulana minyororo yafuchuliwa

Nilipokutana na Ahmed, alikuwa peke yake ndani ya chumba. Alikuwa na alama mwilini mwake kutokana na kuchapo alichokuwa amepewa. Hajui ana miaka mingapi, lakini huenda ana umri wa miaka 10.

 

Shule anayosomea ni moja ya taasisi 23 ya mafunzo ya Kiislamu nchini, ambazo zinajulikana kama khalwas, ambayo nilinasa kanda ya video kisiri katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2018.

Nilishuhudia na kunasa kanda za video za watoto wengi, baadhi yao wana umri wa miaka mitano, ambao wanapigwa vibaya, kufungwa minyororo mara kwa mara na kufungiwa bila kupewa chakula au maji na masheikh wanaosimamia shule hizo. baadhi ya watoto ambao sikuwaangazia katika taarifa hii waliniambia walinajisiwa na kufanyiwa dhulma zingine za kingono.

Kuna karibu taasisi 30,000 za khalwas katika maeneo tofauti nchini, kwa mujibu wa serikali ya Sudan. Zinapokea fedha kutoka kwa serikali na misaada kutoka kwa wahisani ndani na nje ya nchi.

Watoto wanafunzwa kuhifadhi Quran. Kwasababu hazitozi ada yoyote, familia nchingi zinachukulia shule hizo kuwa elimu mbadala ya umma, haswa katika maeneo ya vijijini ambayo hakuna shule zinazoendeshwa na serikali. Wanafunzi huishi huko na kurudi nyumbani wakati wa likizo.

Kwa wengi shule hizo ambazo zimekuwa zikuhudumu kwa miaka na mikaka ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Wasudan, na huchukuliwa kama sehemu ya utambulisho wa kitaifa.

Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni video zinazoonesha watoto wakipigwa katika shule hizo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii, huku taarifa masheikh wanaotuhumiwa kuwabaka wanafunzi ndani ya khalwas zikiangaziwa katika vyombo vya habari nchini Sudan. Lakini Mashirika ya kutetea haki za binadamu zimepuuza madai hayo.

Nilitaka kufichua jinsi unyanyasaji unavyofanyika ndani ya shule hizi, na kuwapa sauti watoto ambao hawana nafasi ya kuelezea kile wanachopitia.

Mimi binafsi nilikabiliwa na hali wanayopita. Nikiwa kijana mdogo, Nilijiunga na khalwa. Kila siku nilikuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu kuepuka kichapo cha waalimu.

Nilijua kuwa nitakosana na marafiki na familia yangu kuhusiana na uchunguzi huu, lakini taarifa hii inastahili kuangaziwa. Nilituhumiwa kuwa sehemu ya “Njama ya magharibi kushambulio elimu ya kidini” na baadhi ya watu miliozungumza nao.

Kufikia wakati niliwasiliana na BBC, Nilikuwa nimenasakisiri kanda za video kwa miezi kadhaa. Katika khalwas ya kwanza niliyozuru ilikuwa inafahamika kama Haj el-Daly, ambako nilisikia watoto wanateswa. Niliingia katika shule hiyo kupitia msikitini na kuswali na wa watu wengine wakati wa sala ya mchana, na kuchukua video kwa kutomia simu yangu wakati nikiendelea na sala.

Nilipopiga magoti nilisikia sauti yakusikitisha. Nilipoangalia juu niliona watoto waliokuwa mbele yangu walikuwa wamefungwa nyororo miguuni kwa pamoja kama wanyama.

Maombi yalipoisha watoto hao walitoka msikitini na kuelekea upande mwingine. Lakini nilipokuwa natoka nilisikia makelele na sauti ya kilio.

(Visited 6 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here