Home Makini Newz ACT Wazalendo yakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

ACT Wazalendo yakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kimeafikia uamuzi wa kujiunga na serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Ado Shaib katibu mkuu wa chama hicho.

Katika mkutano maalum wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo, wameamua kuwa wapendekeze jina la mwanachama atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Pia ACT Wazalendo, imewaruhusu wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge, na madiwani waliochaguliwa kukiwakilisha chama na wananchi waliowachagua.

Miongoni mwa sababu walizotoa kufikia uamuzi huo ni pamoja na kutathmini historia ya mapambano ya demokrasia Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla na kusema kuwa mara nyingi kumejirejelea matukio ya raia kujeruhiwa, uwepo wa uhasama wa kisiasa, kudhalilishwa kijinsia na mali za watu kuharibiwa, huku jambo muhimu ni kuwa na amani.

bendera
Maelezo ya picha,Bendera ya chama cha ACT ikipepea

Aidha, Kamati ya ACT, imeahidi kunafanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Zanzibar ili kurejesha imani ya wananchi juu ya uwepo wa uchaguzi huru na wa haki.

Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, hali ilivyo kwa sasa Zanzibar inahitaji busara kubwa katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi huo, ili kuhakikisha kuwa matukio ya namna hiyo hayajirudii tena.

Chama hicho kimeeleza madhila yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2020, ni watu 17 walifariki dunia.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here