Home Makini Tech MasterCard au Visa? Chaguo sahihi ni lipi? Kadi ipi ni Bora na...

MasterCard au Visa? Chaguo sahihi ni lipi? Kadi ipi ni Bora na Nafuu?

Mastercard au Visa? Ipi ni bora? Kama umeshawahi kutaka kufahamu tofauti kati ya MasterCard na Visa kwenye kadi za ATM za benki na kama kuna manufaa ya kutumia mojawapo dhidi ya nyingine basi makala hii itafungua uelewa wako zaidi.

mastercard au visaJe ushawahi kujiuliza tofauti kati ya MasterCard na Visa?

Makampuni haya yanafanya kazi moja, nayo ni kuwezesha malipo na upokeaji wa malipo kwa watu au wafanyabiashara mbalimbali bila kujali tofauti zao za mashirika/makampuni ya kibenki.

Makampuni haya hayamiliki benki, wala kutoa huduma yao moja kwa moja, wao wateja wao wakuu ni mabenki. Mabenki ndio yanayofanya makubaliano na VISA au MasterCard. Visa na MasterCard wanatoa huduma ya mfumo wa malipo utakaowawezesha wateja wa mabenki husika kunufaika na uwezo wa kufanya malipo kwa njia rahisi ya utumiaji wa kadi zao au taarifa za kinamba zinazokuja kwenye kadi zao.

Tofauti kati kadi za MasterCard na Visa nini?

Tofauti kuu ni za kimfumo, yaani mfumo wa malipo. Hii ni mifumo miwili ya kitofauti ya kimalipo. Mfumo wa mtandao wa malipo wa Visa hautakubali kupokea malipo kutoka kwenye kadi ya Visa na hivyo kadi ya MasterCard itakataliwa na mfumo wa malipo wa Visa.

INAYOHUSIANA  Njia Mpya Na Bora Ya Kuajiri Kutoka ‘BrighterMonday Tanzania’!

Tofauti nyingine ni ya faida tuu ya kadi kwa wateja, sio kadi zote za Visa zinafanana. Na ata kadi za MasterCard sio zote zina sifa moja. Sifa zinaweza kutofautiana ata kwenye kadi za Visa za benki moja, yaani benki moja inaweza inatoa kadi za Visa au MasterCard lakini zikawa na sifa tofauti tofauti.

Je kati ya MasterCard au Visa ni nani mwenye makato makubwa?

Hapa fahamu ya kwamba makato ya utumiaji wa kadi ya Visa au MasterCard hayaamuliwi na makampuni haya. Viwango vya makato vya kadi husika vinaamuliwa na benki inayokupatia kadi hiyo. Mfano kwa makato ya kutoa pesa kwenye ATM au kufanya muhamala mtandaoni yanaweza kuwa tofauti kutoka benki mbili au tatu, kwa kuwa gharama hizo zinawekwa na benki husika na wala si Visa au MasterCard.

INAYOHUSIANA  Mapigo ya moyo kutumika badala ya Alama za vidole! #Usalama

Je unaweza kuchagua aina ya kadi unayotaka ukienda benki?

Ndio. Mabenki mengi yana kadi za aina zote, ila pia kuna mabenki machache yenye kutoa kadi za aina moja tuu. Mara nyingi hii inakuwa kama wameingia mikataba na Visa au MasterCard ambayo inawafanya wapendelee kutoa kadi flani tuu.

Je kadi ipi ndio inakubalika zaidi kwenye malipo?

kadi za visa na mastercard zinapatikana
Sehemu nyingi za malipo; Mtandaoni, Madukani n.k, zinakubali kadi zote mbili

Ni vigumu sana kufika sehemu ambayo kadi moja tuu ndio inakubalika, ni kawaida popote ambapo kadi ya Visa inakubalika kufanya malipo basi utakuta na ya MasterCard pia inakubalika. Watengenezaji wa vifaa vya malipo wengi huweka mifumo yote miwili ili kuwarahisishia wafanyabiashara katika upokeaji wa malipo.

Katika Umaarufu wa kuwa namba moja, kadi za VISA ndio zinazishinda za Mastercard kwa wingi wa wateja katika mataifa mbalimbali duniani

 

Ila kuna kadi ambazo ni maarufu zaidi kwenye maeneo na maeneo kutokana na juhudi za kibiashara za mabenki. Mfano kwa Tanzania kadi za Visa ndio zinatolewa na mabenki mengi zaidi, wakati za MasterCard ukiondoa benki ya NMB ambao walizileta kwa kampeni kubwa, mabenki mengine ni hadi mteja aziulizie – usipoulizia basi moja kwa moja utapewa ya Visa.

INAYOHUSIANA  Nokia Kuingia Ushirika Na Zeiss (Watengenezaji Wa Lenzi Za Kamera)!

Una kadi ya Visa au MasterCard alafu haikubali malipo mtandaoni?

Kuna mabenki yanayotoa kadi hizi na utagundua unaweza kuzitumia popote Tanzania ila pale tuu unapotaka kufanya manunuzi mtandaoni kadi hiyo inakataa. Kadi hizi zinatakiwa ziruhusu malipo sehemu yeyote, ila kutokana na sababu za kiusalama benki yako inaweza ikawa imekupatia kadi huku imezuia uwezo huo. Hivyo ukikutana na changamoto hiyo fika kwenye benki yako kuulizia.

Haya ni machache ya kukufungua zaidi kuhusu kadi hizi. Tunakushauri ni vizuri kupitia taarifa za makato ya huduma tofauti za kibenki ili uweze kufanya maamuzi sahihi pale unapotaka kuwa na kadi ya kibenki ya Visa au MasterCard kwa ajili ya kufanyia miamala mbalimbali. Kumbuka kadi inaweza ikawa ni ya jina moja ila gharama za makato ya miamala ikawa nafuu kwenye benki moja dhidi ya nyingine.

(Visited 2 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here