Home Makini Tech Chanjo ya Korona /Covid19 kuanza kutumika Uiengereza

Chanjo ya Korona /Covid19 kuanza kutumika Uiengereza

Uingereza itakuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutumia chanjo ya korona / Covid19. Chanjo hiyo iliyetengenezwa na makampuni mawili makubwa ya utengenezaji dawa ya Pfizer na BioNTech ina uwezo wa zaidi ya asilimia 95% kumkinga mtu na Korona.

BionTech ni kampuni ya kiteknolojia za sekta ya biolojia ya nchini Ujerumani, huku Pfizer ikiwa ni kampuni ya utengenezaji madawa ya nchini Marekani. Kwa pamoja waliingia katika makubaliano ya kushirkiana katika utengenezaji wa chanjo dhidi ya kirusi cha korona na walipata ufadhili wa kiutafiti kutoka Umoja wa Ulaya, Uingereza na mataifa mbalimbali.

INAYOHUSIANA  Obama aachana na Blackberry yake, akamata simu janja nyingine!

 

chanjo ya korona

Baada tuu ya janga la Korona kuwa kubwa mataifa mengi ya Ulaya, bara la Marekani pamoja na Japani zilianza kutoa pesa za ufadhili wa tafiti za chanjo na tiba kwa makampuni au mashirika yenye uwezo mkubwa wa kiutafiti na utengenezaji wa chanjo na dawa.

Makampuni ya BioNTech na Pfizer yalipata mkataba wa kusambaza dosi zaidi ya milioni 300 za chanjo dhidi ya kovidi kwa Umoja wa Ulaya, milioni 40 kwa Uingereza, milioni 100 kwa Marekani na dosi milioni 120 kwa Japani.

Katika mataifa yote hayo mengine bado vyombo vyao vya kudhibiti ubora vinaendelea kujiridhisha kuhusu usalama wa chanjo hii. Uingereza ndio imekuwa taifa ya kwanza kuipitisha kutokana na kuwa na utaratibu wa haraka na usio na urasimu mwingi ukilinganisha na mataifa mengine.

INAYOHUSIANA  Mwanaume mwenye sura 3: Apatiwa sura mpya mara ya pili

Ndani ya siku chache kuanzia sasa makundi ya wazee, watu wenye matatizo mengine ya kiafya yanayosumbuliwa zaidi na tatizo la Korona ndio yatakuwa ya kwanza kupatiwa chanjo hiyo nchini Uingereza.

Inategemewa katika mataifa mengine hadi kufikia mwisho wa mwaka chanjo hiyo itakuwa imeanza kutumika katika mataifa mengi zaidi. Hii ni habari njema kwa wafanyabiashara na sekta zingine muhimu kama usafiri na utalii kwani hii ina maanisha tutegemee mambo kuanza kurudi sawa mwaka 2021.

(Visited 2 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here