Home Makini Newz WHO yapinga vipimo vya utata vya ‘ubikira’

WHO yapinga vipimo vya utata vya ‘ubikira’

Wanawake wanapewa vipimo vya ubikira vya utata katika kliniki za Uingereza , uchunguzi wa BBC umebaini.

Vipimo hivyo vinadaiwa kuwa vinakiuka haki za binadamu , Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa mataifa(UN) umebainisha, zinataka kiliniki hizo zifungwe.

Wakosoaji wanasema vipimo hivyo haviwezi kudhibitisha kuwa kama ubikira wa mtu unaweza kutajwa kuwa ni unyanyasaji.

Vipimo hivyo vinajumuisha uchunguzi wa uke kama umewahi kuingiliwa.

Uchunguzi wa BBC umebaini idadi kadhaa ya kliniki za binafsi zinazofanya marekebisho ya ubikira, na ukiwasiliana nao unafanyiwa vipimo wanavyoviita vya ubikira vinavyogharimu kati ya paundi £150-£300.

T.I
Maelezo ya picha,Mwaka jana mwanamuziki T.I. alibainisha kuwa amempeleka binti yake ili kufanyiwa vipimo hivyo

BBC iliainisha kliniki 21 na imeweza kufanya mahojiano na kliniki 16 kati yake, kliniki saba zilithibitisha kuwa wanafanya vipimo vya ubikira na baadhi walifafanua nafasi yao.

Wote walisema kuwa walikuwa wanafanya upasuaji wa kurekebisha uke, gharama yake ikiwa kati ya paundi 1,500 mpaka 3,000. Data zinaonesha kuwa walifanya marekebisho wa bikira 69 katika miaka mitano iliyopita.

BBC ilisikia simulizi ya mwanamke mmoja aliyesaidia na asasi ya misaada ya Karma Nirvana, ambayo inasaidia waathirika wanaopitia unyanyasaji na ndoa za kulazimishwa.

“Nilikuwa nanyanyaswa sana na wazazi wangu ambao walitaka niolewe na mtu waliyemtaka yeye,” alisema.

Kukimbia ndio lilikuwa suluhisho pekee kwangu

“Siku moja, kiongozi wa kijiji aliniona na marafiki zangu na alimwambia mama yangu kuwa kati ya wavulana hao mmoja wao alikuwa mpenzi wangu. Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu mimi mtaani kwetu.”

Alitishiwa na wazazi wake kufanyiwa vipimo vya ubikira ili waweze kuhakiki kama bado bikira au la.

“Wazazi wangu na wazazi wa kijana huyo waliotaka niolewe naye walisema wanataka kuhakikisha kama bado niko bikira ili michakato ya harusi iendelee.

“Niliogopa na sikuelewa walikuwa wanamaanisha nini haswa.

Nilihisi kutoroka nyumbani ndio sulhisho – na hicho ndicho nilichokifanya.”

hymen-repair kit including gel, capsules and tweezers
Maelezo ya picha,Kifaa cha kurejesha bikira kinachouzwa mtandaoni

Priya Manota ni meneja wa Karma Nirvana anasema,

“Tumepokea simu kutoka kwa wasichana wenye wasiwasi kuhusu suala hili.

Inawezekana kuwa wanahofia labda wazazi wao watajua kuwa wameingia katika mahusiano na hawako bikira.

Au familia zinawapa msukumo kufanya vipimo hivyo na wana wasiwasi wa matokeo yatakapotoka.

Vipimo hivi vya ubikira vinafanyika katika mataifa yapatayo 20, kwa mujibu wa WHO, ambayo inasema hawana ushahidi kama ina uwezo wa kudhibitisha kuwa msichana ni bikira , au alifanya ngono au hapana.

Hii ni kwa sababu uke unaweza kujifunga kwa sababu nyingi tu ikiwemo mazoezi.

Mwaka jana, mwanamuziki T.I baada ya kukiri kumpeleka mtoto wake kufanyiwa vipimo hivyo kila mwaka kuangalia kama bado hajaanza kuingia kwenye mahusano ya kingono.

Maelezo ya video,‘Alikamatwa na kulazimishwa kufanyiwa vipimo vya ubikira’

Damu feki

BBC imebaini kuwa vifaa vya kurekebisha uke kinauzwa mtandaoni kwa paundi 50, ambacho kinadaiwa kuwa kinarejesha bikira.

Kifaa hicho kimewasili kutoka Ujerumani na kuuzwa kwa paundi 104. Kina milimita 60 ya jeli ya kukaza uke, lailoni na paketi ya damu feki.

Huku hakuna maelezo ya jinsi ya kutumia kifaa hicho.

Dkt Ashfaq Khan huwa anapata anapata maombi ya kurejesha bikira na vipimo vya uwepo wa bikira anasema:

Female doctor with patient, file pic

“Haelewi kwanini vipimo hivyo havikatazwi Uingereza, vinapaswa kukatazwa kisheria,”alisema.

“Wazo la kurejesha ubikira halipo, huo ni uongo mtupu.Ninaweza kukupa cheti lakini cheti hicho kikawa ni cha uogo tu.”

Tuwaeimishe jamii yetu

Anaamini kuwa hatua zaidi zinahtajika dhidi ya zoezi hili.

“Ni sawa na ukeketaji , viongozi ulimwenguni kote wanazungumzia tatizo la ukeketaji na jinsi ya kukabiliana nalo,” alisema.

“Na kwangu mimi huu ni uhalifu – na hayaendani na maadili kabisa.”

Aliongeza “Ni vyema kuwaelimisha jamii yetu kuhusu imani hii potofu ambayo ni biashara tu ila haijali utu.”

(Visited 5 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here