Home Makini Newz Mzozo wa Tigray Ethiopia: Waziri Mkuu Abiy Ahmed ni nani?

Mzozo wa Tigray Ethiopia: Waziri Mkuu Abiy Ahmed ni nani?

“Kwa mtazamo wangu, siamini Ethiopia inahitaji vita. Sitaki kujumuishwa miongoni mwa watu wanaopendelea suluhisho la kijeshi.

Kile ninachotaka kutuma Tigray sio risasi, (afadhali nitume barakoa ambayo inaweza kutumiwa kujikinga dhidi ya) virusi vya corona”.

Hiyo ilikuwa kauli ya Waziri Mkuu Abiy mwezi Septemba wakati jimbo la Tigray linaloongozwa na TPLF iliamua kufanya uchaguzi kupinga amri iliyotolewa na serikali kuu.

Uchaguzi ulikuwa umeahirishwa kutokana na janga la corona.

Wakati huo alisema serikali haitakabiliana kijeshi na jimbo hilo la kaskazini.

Leo Waziri Mkuu anaongoza oparesheni dhidi ya uongozi wa TPLF.

Mzozo huo ambao umeingia wiki ya tatu umeripotiwa kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Mashirika ya kutoa misaada ya binadamu yanasema maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko zaidi ya watu elfu arobaini wakitorokea nchi jirani ya Sudan.

Umoja wa Mataifa umeonya kutokea kwa mzozo wa kibinadamu.

Abiy Ahmed aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia mwezi Aprili mwaka 2018, kufuatia wimbi la maandamano kutoka jamii ya Oromo.

Nchi ilisemekana kuwa katika hatari ya kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwanza wenyewe.

Cheering supporters of PM Abiy

Aliamua kuleta mageuzi makubwa, baadhi ya mageuzi hayo hayakutarajiwa miaka michache iliyopita.

Kwa miaka mingi, serikali ya Ethiopia imekuwa ikikosolewa na makundi ya kutetea haki kwa ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, kuwatenga na kuwafunga viongozi wa upinzani na kutumia nguvu kuvunja maandamano.

Pia ilionekana kupinga uamuzi wa tume ya mipaka ambao ulitarajiwa kukomesha mzozo wa miongo miwili kati yake na nchi jirani ya Eritrea.

Lakini hayo yote yalibadilika Abiy alipoingia madarakani. Alikubaliana na uamuzi huo na kufikia mkataba wa amani na Eritrea.

Uamuzi huo wa kihistoria ulimwezesha kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019.

Alionekana kujitolea kikamilifu kufikia amani na ‘maadui’ wa watangulizi wake.

Baba yake Ahmed Ali ambaye alifariki dunia mwaka mmoja baada ya yeye kuwa waziri mkuu alimuelezea kama ”mtoto ambaye alikuwa rafiki wa kila mtu ,” katika mahojiano na BBC mwezi Julai mwaka 2018.

Abiy Ahmed ni nani?

Abiy Ahmed at a rally

Historia ya Bwana Abiy ni muhimu katika kutathmini jinsi watu wanavyomchukulia.

Ni kiongozi wa kwanza kutoka jamii ya Oromo nchini humo – Kabila ambalo liliongoza maandamano ya kupinga serikali kwa karibu miaka mitatu, na kusababisha vifo vya watu kadhaa na maelfu ya wengine kukamatwa kufuatia makabiliano na vikosi vya usalama.

Moja ya malalamiko makuu ya waandamanaji ni kwamba wametengwa kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miaka mingi- licha ya kuwa jamii iliyo na watu wengi zaidi nchini humo.

Bwana Abiy alipoingia madarakani, hayo yote yalainza kubadilika.

Aliwahi kuwa kuwa kiongozi wa Oromo People’s Democratic Organisation (OPDO), moja wapo wa vyama vinne vikuu vya kijamii ambavyo viliungana kubuni muungano wa chama tawala cha Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front (EPRDF) .

Mwezi Desemba mwaka jana, Bwana Abiy alivunjilia mbali EPRDF ambayo imeongoza siasa za Ethiopia kwa karibu miongo mitatu, na kubuni chama kimoja cha kitaifa, Prosperity Party, chama ambacho TPLF ilikataa kujiunga.

he leader of the "Oromo Peoples Democratic Organization" (OPDO) Abiy Ahmed looks on during a news conference in Aba Geda, Ethiopia, 02 November 2017

Waziri Mkuu huyo aliye na umri wa miaka 44 – alizaliwa katika mji wa Agaro ulioko jimbo la Oromia anatoka katika familia mchanganyiko wa Wakristo Waislamu, alijiunga OPDO mwishoni mwa miaka ya 1980.

Katika jeshi alipanda madaraka na kufikia cheo cha luteni kanali, kabla ya kuwa mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la mawasiliano na usalama, mtandao ambao jukumu lake lilikuwa kutoa huduma ya usalama wa kimtandao katika nchi ambayo serikali inadhibiti vikali intaneti.

Baada ya hapo alikuwa waziri wa sayansi na teknolojia.

Ameahidi kuweka mabadiliko katika mawasiliano ya simu, ambayo ambayo kwa sasa inaendeshwa na serikali.

Presentational grey line

Maelezo muhimu: Abiy Ahmed

Abiy Ahmed

Alizaliwa mjini Agaro kusini mwa Ethiopia mnamo Ahosti 15, mwaka 1976 katakana na baba Muoromo Muislamu na mama Mkristo kutoka jamii ya Amharic.

Mwaka 1990 akiwa kijana barobaro, alijiunga na harakati za kijeshi dhidi ya utawala wa kimila wa Derg.

Ana shahada ya uzamili ya masuala ya Amani na usalama kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa na shahada ya uzamili ya katika masala ya uongozi kutoka chuo kikuu cha Greenwich, London.

Anazungumza lugha ya Kioromo, Amharic ,Tigrinya, na Kiingereza.

1995: Alihudumu kama Mlinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda

2007: Alibuni shirika la Ethiopia la mawasiliano na usalama wa mtandaoni (INSA) na kuhudumu kama mwanachama wa bodi ya Ethio Telecom, Ethiopian TV

2010: Aliingia katika siasa kama mwanachama wa kawaida wa OPDO kabla ya kujiunga na makakati juu ya chama hicho mwaka 2015

2016: Alihudumu kwa muda mfupi kama waziri wa sayansi na teknolojia.

2018: Alikuwa Waziri Mkuu

2019: Aliunganisha muungano wa chama tawala EPRDF, ikuwa chama kimoja – cha Prosperity Party.

2019: Alishinda Tuzo ya Amani ya NobeL.

2020: Alitangaza operesheni ya kijeshi dhidi ya TPLF

line

Tuzo ya Amani ya Nobel:

Mkataba wa amani uliofikiwa na Bwana Abiy na Eritrea ulimaliza mgogoro wa mpakani wa miaka 20- ulisbabisha vita vya mpaka kuanzia mwaka 1998-2000.

Alitangazwa kuwa mshindi wa 100 wa Tuzo ya Amani ya Nobel mjini Oslo, ambako alipokea tuzo yake mwezi Desemba mwaka 2019.

nobel

Katika hotuba yake mjini Oslo, alisema:

“Inachukuwa watu wachache kuanzisha vita. Lakini inachukuwa kijiji na nchi nzima kuleta amani.

Kwangu mimi kukuza amani ni sawa na kupanda na kukuza miti. Sawa na miti inavyohitaji maji na mchanga wenye rutuba kukua, amani inahitaji kujitolea,kuwa na subira na utashi wa kudumu ili kupata manufaa yake.”

Baada ya kupewa tuzo hiyo baadhi ya watu waliwasiliana na makati ya inayoandaa tuzo hiyo mjini Oslo na kusaini liana ya kutaka tuzo hiyo kutenguliwa, kutokana na ” visa vya baadhi ya Waethiopia kutoweka na wengine kuuawa.”

Hali ambayo iliilazimu kamati ya Nobel ya Norway kutoa taarifa. Inasema ”Tunasimama kidete na uamuzi wetu wa mwaka jana wa kumpatia tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019 Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Abiy Ahmed.Kamari hiyo haijawahi kubali msimamo wake, lakini kwa sasa, ina nia yoyote ya kufanya hivyo.”

Nataka kusema ”Ukweli ni kwamba,kulingana na kanuni ya kamati ya Nobel Tuzo ya Amani ikitolewa haiwezi kutenguliwa.”

Neno Medemer limekuwa maarufu sana nchini Ethiopia.

majeshi

Neno hilo kwa lugha ya Kimhara linamaanisha ”kuongeza” lakini pia linatafsiriwa kama “kuja pamoja”, hali ambayo inaelezea jinsi waziri mkuu Abiy anavyoshughulikia changamoto zinazoihusu Ethiopia kwa njia ya kipekee.

Neno hilo aidha limekita mizizi baada ya waziri mkuu kuandika kitabu kilicho na neno hilo kilichozinduliwa katika hafla ya kufana mwezi oktoba katika miji tofauti nchini Ethiopia.

Inaripotiwa kuwa maelfu ya nakala za kitabu hicho zimechapishwa katika nchi hiyo ambayo lugha zinazozungumzwa zaidi ni Amharic na Afaan Oromoo.

Katika kitabu hicho chenye sura 16 na kurasa 280, Abiy anaangazia maono yake anayosema yamekuwa muongozo wa maisha yake tangu akiwa mtoto.

Bwana Abiy anataka Ethiopia iwe na mshikamano wa kitaifa licha ya kwamba inakabaliana na mgawanyiko wa kikabila lakini pia anataka tofauti iliopo iwe yenye kufurahiwa na kila mmoja.

Mafanikio yake katika kuhakikisha taifa linafanikiwa itakuwa jambo la msingi katika muda atakaokuwa madarakani.

Kitovu cha falsafa hii ni dhana ya kwamba, watu wanaweza kuwa na maoni tofauti lakini maridhiano yakapatikana.

Tangu alipoingia madarakani, ni wazi kwamba uongozi wa Bwana Abiy umekuwa tofauti kabisa na uliokuwepo katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita.

Amejitahidi kuondoa msimamo mkali katika masuala ya kiusalama na kukumbatia njia za mazungumzo ya uwazi na kwa uhuru katika siasa.

Amesema kwamba watangulizi wake walijaribu kutumia mbinu za usawa na kupitisha kila kitu katika serikali kuu kuhusu masuala ya kiuchumi lakini wakashindwa kwa sababu ukosefu wa uelewa mzuri wa Ethiopia.

Mzozo wa Tigray:

Mzozo ulianza Novemba tarehe 4, 2020, baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuamuru oparesheni ya kijeshi dhidi ya vikisi vya jimbo la Tigray.

Alisema amechukua hatua hiyo kujibu mashambulio dhidi ya kambi ya jeshi la taifa katika jimbo laTigray.

“Serikali ililazimika kuchukua hatua ya kijeshi,” Bwana Abiy alisema.

____

Athari za kikanda:

Celebrations as border is reopened

Katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita akiwa madarakani, Bwana Abiy amekuwa kiungo muhimu katika juhudi za muleta Amani katika maeneo mengine yanayokumbwa na mgogoro wa kikanda.

Alikuwa kiungo muhimu katika mchakato wa kuleta utawala wa kijeshi nchini Sudan katika meza ya mazungumzo na upinzani kufuatia maandamano yaliyokumba Khartoum na miji mingine.

Mazungumzo hayo yalichangia kubuniwa kwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.

Kando na hayo alisaidia katika juhudi zakufufua uhusiano wa kidiplomasia kati ya Eritrea na Djibouti baada ya uhasama wa kisiasa wa miaka miwili.

Bwana Abiy pia amekuwa mpatanishi wa Kenya na Somalia katika mzozo wa mpaka wa majini kati ya nchi hizo mbili.

Na pia amehusika katika mazungumzo ya amani kati ya Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Abiy ametaja oparesheni ya kijeshi inayoendelea kuwa ‘utekelezaji wa sheria’ na amekataa juhudi za upatanishi za kigeni.

Wiki hii alitangaza ‘awamu ya mwisho’ ya oparesheni inayolenga kuteka mji mkuu wa Tigray, Mekelle.

Matokeo ya makabiliano haya ya kijeshi dhidi ya ‘wakuu wa Tigray’ kama anavyosema itaamua ikiwa atabadilisha mbinu yake ya kukabiliana na changamoto zinazokumba Ethiopia.

Je ataendelea na sera yake ya mabadiliko ama atabadili mtindo wake wa utawala?

(Visited 4 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here