Home Makini Buzz Ufunguzi wa kambi ya Miss Tanzania 2020 yaanza rasmi

Ufunguzi wa kambi ya Miss Tanzania 2020 yaanza rasmi

Waandaji wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kampuni ya The Look wamefungua kambi ya Miss Tanzania ambayo inaanza leo Novemba 26 na kufikia tamati Desemba 05 mwaka huu.

 

Akizungumza na Waandshi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mkuu wa The Look  Bi. Basilla Mwanukuzi Shayo amesema mwaka 2020 walifanya mchakato wa washiriki kwa kutumia mfumo wa usaili (Audition) katika kanda 6 za Tanzania  ambazo ni  kanda ya kati, kanda ya Ziwa,Kanda ya Kaskazini,Kanda ya Mashariki , Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Dar es Salaam.

“Kutoka katika kanda hizo jumla ya washiriki 20 walipatikana na leo hii ndio wameanza kambi maalumu ya mchakato wa kumpata mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2020”. Amesema Bi.Basilla.

 

Aidha Bi.Basilla amesema kila mshiriki alitakiwa kuandaa mradi (Project) iwapo atashinda taji la Miss Tanzania 2020 basi atatumia Mradi huo kuupeleka katika Mashindano ya urembo ya Dunia ambapo Miradi mingi hushindanishwa katika kipengele cha Mrembo na Malengo.

 

 

 

“Washiriki wote hawa 20 wanayo miradi yao na mmoja wao atakaeshinda taji la mremb o wa Taifa Miss Tanzania 2020 atatuwakilisha yeye na project yake hiyo”. Ameeleza Bi.Basilla.

(Visited 9 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here