Home Makini Newz Janice Bryant: Mfahamu mwanamke wa kwanza mweusi kuwa bilionea Marekani na mafanikio...

Janice Bryant: Mfahamu mwanamke wa kwanza mweusi kuwa bilionea Marekani na mafanikio yake

Janice Bryant Howroyd alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa na biashara yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja nchini Marekani.

Akilelewa kusini mwa nchi hiyo,wakati wa ubaguzi wa rangi alikumbana na matatizo mengi akiwa anatafuta kazi hivyobasi, alitumia uzoefu wake kama muongozo alipoamua kuanza kampuni yake ya raslimali watu.

Uamuzi uliomfanya kuweka historia.

Akifanya mahojiano na BBC, Janice alizungumzia taaluma yake.

Janice Bryant Howroyd alikuwa kusini mwa Marekani katika jimbo la North Carolina miaka ya 1950, wakati kulipokuwa na ubaguzi wa rangi.

Lakini kulingana na wazazi wake, maisha yake na ndugu zake wengine 10 hayangeendeshwa na ubaguzi wa rangi.

“Mama yangu na baba yangu sio kwamba walikuwa wamesoma sana, lakini walikuwa werevu mno,” anasema.

“Walinifunza kuwa nina haki sawa kama mwingine yoyote yule, pengine sio kwa fursa zote lakini mimi ndio nilihitajika kutengeneza fursa hizo”.

Pia walinifunza nisitafute fursa hizo kwa uchungu ili hasira isiwe sehemu ya maisha yangu. Kikubwa ya nilichofikia ni kitaaluma na maisha yangu binafsi kutokana na kile nilichojifunza mwanzoni nyumbani, “ameongeza.

Wakati huo, sheria zinazotenganisha watu weusi na wazungu zilikuwa bado zinatumika, zilianza kutekelezwa baada ya kukomeshwa kwa utumwa.

“Nisingemuoa mume wangu na macho yake mazuri ya Buluu, wakati huo,” anasema.

Sheria za ubaguzi zilipoanza kufutwa baada ya kujitokeza kwa vuguvugu za kupigania haki za raia.

Janice alikwenda kusoma katika shule ambayo ilikuwa inatekeleza mchakato wa kurejesha mambo sawa na huko ndipo alipokutana na wanafunzi wazungu katika darasa moja.

“Siku ya kwanza, nikitembeatembea chuoni nilikuwa na wasiwasi sana. Ilikuwa vigumu kwangu hata kusikia kinachoendelea darasani kwasababu hofu iikuwa imenijaa. Bado sijaelewa namna ya kuelezea nilivyokuwa ninahisi siku ile,” anasema.

Bryant Howroyd alikulia wakati ambapo kulikuwa na matatizo mengi ya kibaguzi
Maelezo ya picha,Bryant Howroyd alikulia wakati ambapo kulikuwa na matatizo mengi ya kibaguzi

Wakati kukiwa na ukosefu wa usalama na unyama unaotendeka barabarani, anasema kuwa kaka zake walimpeleka shuleni kila siku. Lakini baada ya kwenda chuo, akaanza kuhisi yuko nyumbani.

Alihudhuria chuo cha A&T North Carolina, moja ya vyuo vya kihistoria vya watu weusi nchini humo.

“Nilijifunza Kiingereza na somo la huduma za Jamii. Ni taasisi ya kupigiwa mfano. Baadaa ya vita vya weyewe kwa wenyewe kulianzishwa baadhi ya shule na taasisi za wanafunzi weusi. Na hapo ndipo kulipobainika mwanaangana wa kwanza mweusi na viongozi wengine weusi nchini humo,” anasema.

Ujasiriamali

Mwaka 1976, alihamia Los Angeles, California, kufanyakazi kwa muda tu kama msaidizi wa shemeji yake Tom Noonan katika kampuni ya jarida la Billboard.

Janice anakumbuka kwamba mkuu wa kampuni alilazimika kusafiri kuhudhuria mkutano mmoja Ulaya na yeye akaachiwa fursa ya kusimamia kampuni.

“Aliporejea, alipata ofisi imebadilika sio ile alioiacha na kuiona ikiwa bora zaidi. Nakumbuka akisema nimefanya miujiza,” Janice alisema.

Hapo ndipo shimeji yake alipobaini kipaji chake na kumsihi kuendelea kutimiza ndoto yake. “Tom ndio sababu ya mimi kuendeleza taaluma yangu ya ujasiriamali na nikaamua kufungua biashara,” anasema Janice.

Kile ambacho watakuja kukisoma kunihusu siku zijazo sijafanya aliusema mwanamke huyo
Maelezo ya picha,Kile ambacho watakuja kukisoma kunihusu siku zijazo sijafanya aliusema mwanamke huyo

Mwaka 1978, miaka miwili baada ya kuwasili Los Angeles, Janice alianzisha mapuni ya yake ya ActOne.

“Naweza kusema kuwa uzoefu wangu wa kutafuta kazi ni jambo ambalo sikutaka limtokee mwingine yeyote. Kwahiyo, nilipoanzisha kampuni yangu nilijua kuwa nataka kuendeleza ubinadamu katika taaluma ya raslimali watu.

Anasema alianza biashara yake na dola 1,500 pekee. “Nilikuwa na dola 900 na nikaomba dola mia 600 kutoka kwa mama yangu,” anasema.

Kampuni hiyo ilikuwa na mashine moja tu ya fax na simu pekee.

Billionaire

Miaka 40 baadaye, Kampuni ya ActOne inapatikana katika nchi 19, na inahudumia zaidi ya wateja 17,000 na imeajiri watu 2,600.

Hata hivyo uongozi wa kampuni hiyo unasema, kufikia lengo hilo hakukuwa ndoto yake. “Kama mjasiriamali, (lengo langu) ni kufikia watu biloni 2,” anasema.

Kilichompa motisha

Akiwa katika safari yake hii, Janice anasema mama yake amekuwa nguzo muhimu katika kutimiza ndoto yake.

Na aliposhinda tuzo ya ujasiriamali, Janice alimuita mama yake jukwaani, kuhutubia hadhira na kumshukuru Mungu.

Lakini je nini kinamfanya kuendelea kung’ara katika taaluma yake?

“Hata ninaposhinda matuzo, huo sitoi fursa kwa umaarufu kudhibiti maisha yangu,” Janice amesema.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here