Home Makini Newz Ahadi ya Spika Job Ndugai kwa wabunge wa Chadema

Ahadi ya Spika Job Ndugai kwa wabunge wa Chadema

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa wabunge 19 wa Viti Maalum Chadema walioapishwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Jumanne Novemba 24, 2020.

 

Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge hao, Ndugai ameeleza kuwa atawapa ushirikiano wote ili waweze kutimiza majukumu yao.

“Neno langu kwenu nendeni mkawatumikie  watanzania, naahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ya wabunge wachache wajibu wa spika ni kuwalinda walio wachache.”

“Nitajitahidi kuwalinda kuwapa haki  ili muweze kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania na muweze kufanya kazi yenu ya kikatiba kwa ukamilifu,” amesema Ndugai.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here