Home Makini Tech Elon Musk ampiku Zuckerberg, Sasa hawa Tajiri Namba Tatu Duniani

Elon Musk ampiku Zuckerberg, Sasa hawa Tajiri Namba Tatu Duniani

Elon Musk ampiku Zuckerberg kwenye orodha ya matajiri wakubwa duniani. Kwa sasa Bwana Elon Musk anashikilia nafasi ya tatu duniani.

Elon Musk
Bwana Elon Musk, mbele ya gari la CyberTruck. Moja ya gari lililo jikoni kwa sasa katika kampuni ya Tesla

Wiki hii chombo cha habari cha Bloomberge kimepandisha Elon Musk kwenda nafasi ya tatu kutokana na kutambulika kwa mafanikio makubwa kwa kampuni yake ya utengenezaji magari yanayotumia umeme, Tesla, kampuni hiyo imefanya vizuri katika soko la hisa na kuchangia utajiri wa Bwana Musk kukua kwa dola bilioni 12 wiki hii.

 

Elon Musk ampiku Zuckerberg
Elon Musk ampiku Zuckerberg na kuchukua nafasi ya tatu duniani. Katika kipindi cha miezi 12 utajiri wa Bwana Musk umekua kwa zaidi ya dola bilioni 92. Data hizi ni za 19 Novemba, kwa sasa utajiri huo umefikia dola bilioni 144.

 

Kutokana na ongezeko la utajiri wa dola bilioni 12 za Kimarekani, kwa sasa kwa ujumla wake Bwana Elon Musk anautajiri wa zaidi ya dola bilioni 144 kulingana na taarifa za kampuni ya habari na tafiti ya Bloomberg. Kutokana na ongezeko hilo la utajiri Bwana Elon Musk ameichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na muanzilishi wa Facebook, Bwana Zuckerberg kwa muda mrefu.

INAYOHUSIANA  Sababu 5 kwanini ndege inapata ajali

Elon Musk ni nani?

Elon Musk ni mfanyabiashara na mbunifu mzuri wa miaka yetu. Alianza kupata lengo la uwekezaji mkubwa baada ya kunufaika na mauzo ya kampuni ya Paypal kwenda kwa Ebay, Elon alikuwa muwekezaji na alishaongeza kampuni ya Paypal kwa kipindi flani. Mwaka 2002 Paypal ilipouzwa kwenda kwa Ebay, ELon alipokoa dola milioni 165 kama malipo kwa kuwa mmiliki wa asilimia 11.7 ya kampuni hiyo.

Mwaka 2002 alianzisha kampuni ya masuala ya anga inayokwenda kwa jina la Space X ambayo imeanza kupata mafanikio makubwa hivi karibuni katika masuala ya anga. Soma habari za Space X hapa 

INAYOHUSIANA  Makazi binafsi katika anga kuja – #Teknolojia
elon Musk na Space X
SpaceX imekuwa kampuni ya kwanza binafsi duniani kufanikisha safari za wanaanga kwenda kituo cha anga cha kimataifa (ISS)

 

2015 alitengeneza kitengo spesheli ndani ya kampuni ya Space X kinachotambulika kwa jina la Starlink kikiwa na lengo la kuanzisha huduma ya intaneti ya kasi kwa kutumia mfumo wa satelaiti katika anga ya chini ya dunia. Tayari Starlink imeanza kutoa huduma hiyo kwa majaribio nchini Marekani, itakapokamilika mtu yeyote ataweza kupata huduma ya intaneti ya kasi eneo lolote la dunia. Watafiti wengi wanaamini huduma hii itakuja kuwaletea pesa nyingi sana.

2004 aliingia kwenye kampuni ya utengenezaji magari ya kisasa ya mfumo wa umeme ya Tesla iliyokuwa imeanzishwa mwaka 2003. Kuingia kwake kulileta mabadiliko makubwa na chini ya uongozi wake kama Mkurugenzi Mkuu kampuni hiyo imeendelea kukua, hadi sasa yeye ndio Mkurugenzi aliyedumu kwa muda mrefu zaidi katika makampuni ya magari.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Hizi ni sehemu tuu zinazochangia sehemu ya utajiri wake, ingawa hapokei mshahara kutoka kampuni ya SpaceX ila Bwana Elon Musk anapatiwa marupurupu mengi na kuzawadiwa umiliki kupitia soko la hisa pale mafanikio yanapotokea kwenye makampuni haya. Kwa mwaka huu tuu hadi sasa utajiri wake umekua kwa zaidi ya bilioni 82. Hivyo huu hakika ndio mwaka wa mafanikio mengi kwa makampuni anayojihusisha nayo, hasa hasa SpaceX.

Bwana Zuckerberg anachukua nafasi ya nne akiwa na utajiri wa dola bilioni 103. Kumbuka dola bilioni 1 ni takribani Tsh Trilioni 2.3.

(Visited 3 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here