Home Makini Newz Chui atembea umbali mrefu kutafuta jike la kumpanda

Chui atembea umbali mrefu kutafuta jike la kumpanda

Ametembea mwendo mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa na chui nchini India kupata “makazi” katika hifadhi ya wanyamapori.

Mnyama huyo dume ambaye anafahamika na kwa jina maarufu Walker miongoni mwa maofisa wa wanyamapori, sasa ana miaka mitatu na nusu na alitoka katika hifadhi ya wanyamapori ya jimbo la Magharibi la Maharashtra mwezi Juni mwaka jana. Huenda alikuwa anatafuta chakula, mahali pengine pa kuishi au jike wa kuzaa naye.

Akiwa amevishwa kifaa maalum cha kubaini alipo shingoni, alitembea mwendo wa kilomita 3,000 sawa na (maili 1,864) kupitia wilaya saba za Maharashtra na jimbo jirani la Telangana kwa zaidi ya miezi tisa na hatimaye “kutulia” katika hifadhi nyingine mjini Maharashtra mwezi Machi. Kifaa hicho kilitolewa katika shingo yake mwezi Aprili.

Hifadhi ya Dnyanganga iliyo na ukubwa wa kilomita 205 za mraba ni makazi ya wanyama wa kila aina. Lakimni Walker ndiye chui pekee anayeishi hapo, wanasema afisa wa wanayamapori.

“Hana tatizo la himaya yake. Na ana sehemu kidogo ya kutafuta chakula,” Nitin Kakodkar, afisa wa ngazi ya juu wa katika jimbo la Maharashtra aliambia BBC.

Sasa maofisa wa wanyamapori wanatafakari uwezekano wa kumleta chui wa kike ili kumpatia Walker mwenza wa kuzaa naye, hatua ambayo huenda “isiyo ya kawaida”.

Chui sio wanyama ambao unaweza kung’amua wanapotaka kuwa na jike , wanasema, na kwamba wana njia asilia ya kutafuta mke. Kando na hilo itakuwa vigumu sana kumhamisha chui kutoka hifadhi moja hadi nyingine.

“Sababu moja, ni kwamba sio hifadhi kubwa. Imezungukwa na mashamba na misitu iliyoharibiwa. Pia endapo Walker atazalia hapa, kutakuwa na changamoto ya kutafuta chakula hasa miongoni mwa chui wadogo ambao pia wataanza kutawanyika,” Bw Kakodkar alisema.

India inakadiriwa kuwa makazi ya 70% ya chui duniani

India ina asilimia 25 ya makazi ya chui lakini inachangia asilimia 70 ya chui wa porini, na wanyama karibu 3,000. Idadi ya chui imeongezeka, lakini makazi yao asilia yamesalia ilivyokuwa kitambo,wanasema wataalamu.

Kila chui anahitaji kuzalia mahali ambapo ataweza kupata chakula kwa urahisi kama wanyama 500 hivi kuhakikisha wanapata “akiba ya chakula”, wanasema wataalamu.

Walker alivishwa kifaa maalumu cha kufuatilia anaconda mwezi Februari mwaka uliopita na aliendelea kutembea kutoka msitu mmoja hadi mwingine hadi msimu wa mvua ulipowadia “kupata mahali pazuri pa kuishi”.

Maofisa wa wanyamapori wanasema wanyama familia ya paka wakubwa hawatembei kwa “mstari mmoja”. Mwendo wake ulifuatiliwa kupitia mtambo wa GPS na taarifa zake kunakiliwa katika maeneo 5,000.

Wakati wa msimu wa baridi kali na sehemu ya msimu wa joto, Walker alionekana akizunguka katika mashamba akienda mbele na kurudi nyuma mara kwa mara, katika kingo za mito na Barabara kuu.

Mwendo huo mrefu unaashiria nini?

Msimu wa baridi ni wa kupanda pamba katika jimbo la Maharashtra, na mimea humsaidia mnyama huyo kujificha anapotembea kupitia mashamba ya watu. Mara nyingi alikuwa akitembea nyakati za usiku, akiua nguruwe wa porini na ng’ombe kama chakula.

Alikorofishana na wanadamu mara moja alipomjeruhi kwa bahati mbaya na baada ya watu wakafuata nyayo zake hadi mahali alipokuwa anapumzika kichakani. Mtu huyu aliachwa na majeraha madogo.

“Kile ambacho mwendo huo wa muda mrefu kinaashiria ni kwamba licha ya maendeleo na ongezeko la idadi ya watu, maeneo ya vijijini katika jimbo la Maharashtra bado ni mazingira mazuri kwa wanyama kutembea kwa uhuru.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here