Home Makini Tech Nokia 6300 4G na Nokia 8000 4G, Simu nzuri za bei nafuu...

Nokia 6300 4G na Nokia 8000 4G, Simu nzuri za bei nafuu zinazokuja na 4G na apps mbalimbali

Nokia Mobile wametambulisha simu mpya mbili wiki hii, nazo ni Nokia 6300 4G na Nokia 8000 4G. Hizi ni simu mpya ambazo bado zinatuletea yale maumbo ya simu zilizofanya vizuri sana miaka ya nyuma kutoka Nokia.

Tofauti kuu kwa sasa hizi ni simu mpya na ni za kisasa kwenye eneo la kiteknolojia.Ingawa simu hizi zinakaa katika familia ya simu za bei nafuu na hazibebi sifa nzima za kuwa ‘simu janja/smartphone’, bado ni simu zenye uwezo mkubwa wa kimawasiliano na hii ikiwa ni pamoja na kuja na apps muhimu za kimawasiliano kama vile WhatsApp, Facebook na Twitter.

 

Kitaalamu simu hizi zinabeba sifa ya kuitwa ‘featured phones’, yaani ni simu zenye uwezo mzuri lakini kiutendaji bado zipo nyuma kidogo ya simu janja/smartphones.

Simu za Nokia 6300 4G na Nokia 8000 4G
Toleo la 6300 4G kushoto, na toleo la Nokia 8000 4G kulia.

Simu zote zinatumia programu endeshaji ya familia ya Linux, ya KaiOS inayotengenezwa spesheli kwa ajili ya simu za sifa ya featured phones huku ikizipa uwezo wa utumiaji wa apps mbalimbali muhimu ambazo pia hupatikana kwenye simu janja – tofauti hapa ni kwamba apps hizi zinatengenezwa spesheli kwa ajili ya ajili ya programu hii isiyohitaji vipuri vya bei ghari ili kuweza kufanya kazi.

Nje ya Facebook, na WhatsApp pia simu hizi zinakuja na apps kama vile YouTube, Google Maps, Google Assistant.

Simu ya Nokia 6300 4G.

Simu ya Nokia 6300 4G
Simu ya Nokia 6300 4G

Hii ni simu ya bei nafuu zaidi kati ya hizi mbili ingawa bado bei haijawekwa wazi. Ina beba umbo/body la plastiki na ina patikana katika rangi kadhaa kama vile ya kijani, ya majivu na nyeupe.

Sifa zake zingine:

  • Ina display ya ukubwa wa inchi 2.4 kwa skirini ya teknolojia ya  QVGA
  • Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 210 ikiambatanishwa na RAM ya MB 512
  • Diski Ujazo wa GB 4 na uwezo wa kuongeza kupitia memori kadi
  • Uwezo wa betri wa mAh 1500
  • Kamera ya Megapixel 0.3
INAYOHUSIANA  ‘Surface’, Microsoft Waamua Kutengeneza ‘Tablet’!

Pia simu hii inakuja na uwezo wa laini mbili, LTE/intaneti ya 4G, teknolojia ya Bluetooth, WiFI na uwezo wa kutengeneza Hotspot ya Wifi, na FM Redio.

Simu ya Nokia 8000 4G

Simu ya Nokia 8000 4G
Simu ya Nokia 8000 4G

 

Hii ata kimuonekana inategemewa kuwa ni ya bei ya juu ukilinganisha na Nokia 6300 4G ila kuna tofauti ndogo kwenye uwezo wa simu hizo.

Sifa za Nokia 8000 4G

  • Display/Inaukubwa wa inchi 2.80
  • Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 210 ikiambatanishwa na RAM ya MB 512
  • Diski Ujazo wa GB 4 na uwezo wa kuongeza kupitia memori kadi
  • Uwezo wa betri wa mAh 1500
  • Kamera ya Megapixel 2

Pia simu hii inakuja na uwezo wa laini mbili, LTE/intaneti ya 4G, teknolojia ya Bluetooth, WiFI na uwezo wa kutengeneza Hotspot ya Wifi, na FM Redio.

Ukiacha kuwa Nokia 8000 4G ina umbo kubwa zaidi ya Nokia 6300 4G na tofauti katika kiwango cha kamera, Nokia wamewekeza zaidi katika kuipa Nokia 8000 4G muonekano ulio bora na kuwavutia zaidi ukilinganisha na nokia 6300 4G.

Kwenye Bei

Nokia 6300 4G inategemewa kupatikana kwa bei isiyopungua dola 58, yaani takribani Tsh 140,000/= , wakati Nokia 8000 4G inategemewa kupatikana kwa si chini ya dola 93 yaani takribani Tsh 220,00/=. Ila kumbuka bei inaweza kuwa juu kwa Tanzania kwa sababu za kikodi na kibiashara.

Je una mtazamo gani juu ya simu hizi mbili za bei nafuu?

(Visited 2 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here