Home Makini Buzz Kifo cha Ginimbi: Genius Kadungure, umiliki wa nyoka na utata mwingine kuhusu...

Kifo cha Ginimbi: Genius Kadungure, umiliki wa nyoka na utata mwingine kuhusu chanzo cha utajiri wake

 

Genius Ginimbi showcase im cars

Kifo cha mzimbabwe aliyekuwa maarufu sana katika mitandao ya kijamii wa Zibabwe mwenye umri wa miaka 36 na mfanyabiashara , Genius Kadungure a al maarufu Ginimbi kilichotokea tarehe 8 November kimeibua utata miongoni mwa watu wengi huku watu katika mitandao ya kijamii wakijiuliza chanzo cha utajiri wake.

Baadhi ya watu wamediriki hata kusema kuwa alikuwa na nyoka ambaye alikuwa akimtemea pesa; lakini baadhi ya marafiki wa Ginimbi wamejitokeza na kumtetea wakisema kuwa ni kwanini watu hawakujiuliza chanzo cha utajiri wake wakati alipokuwa hai?

Mmoja wa marafiki wake, Ronald Muzambe amesema katika taarifa yake : “kila mtu anayemfahamu Ginimbi hadi alipofikia umri wa miaka 36 anamuelewa kuwa alikuwa na vyanzo vingi vya utajiri. Hakuna yeyote ambaye alishawahi kuuliza ni vipi alipata utajiri alipokuwa hai, ni kwanini wanaongea mambo tofauti kumuhusu wakati sasa amekufa ?”

Muzambe anasema watu wamuache marehemu afe kwa amani. Ninawashauri watu “wawe na hisia za kiutu angalau kidogo ili kumuaga vizuri na kuonyesha heshima kwa rafiki zake na familia yake katika wakati huu mgumu .”

Genius Ginimbi showcase im cars

Ginimbi amekuwa maarufu tangualipokuwa na umri wa miaka 26 akiwa muuzaji wa gesi ya petroli (LP) . Tangu wakati huo alikuwa ni aliyependa kujifurahisha na marafiki zake kwa kufanya sherehe ndogo ndogo za mara kwa mwara wakati ule, kabla ya kuanza kufanya sherehe kubwa.

Magari ya Ginimbi

Kwa miaka mingi , amekuwa akimiliki magari ya garama kubwa na hakuficha wakati wowote kuonesha kila gari alilonunua kupitia mitandao ya kijamii.

Genius Ginimbi showcase im cars

Kabla ya kihfo chake, alikuwa ndio tu amenunua gari jipya la Lamborghini Aventador ambalo alilielezea kama kitu kipya cha kuchezea(new toy).

Kulingana na gazeti la Times Live, miongoni mwa magari yake ambayo ameyaacha ni pamoja na :

 • Rolls-Royce Ghost (2016 model)
 • Rolls-Royce Ghost (2020 model)
 • Rolls-Royce Wraith (ambalo alikufa akiwa analiendesha)
 • Bentley Continental GT (2014 model)
 • Bentley Continental GT W12 (2020 model)
 • Bentley Bentayga
 • Bentley Mulsanne
 • Lamborghini Aventador S Coupe
 • Ferrari 488 Spider
 • Mercedes G Wagon Brabus (2016 model)
 • Mercedes G Wagon G63 (2020 model)
 • Range Rover Vogue Autobiography (2019 model)
 • Range Rover Sport SVR (2019 model)
 • Range Rover Sport Lumma (2017 model)
 • Range Rover Sport (2018 model)
 • Range Rover Velar (2018 model)
 • Mercedes-Benz S Class (2014 model)
 • Mercedes-Benz S Class (2019 model)

MAKINI BUZZ Hata hivyo haikuweza kupata chanzo huru cha kuthibitisha taarifa zilizotolewa na gazeti la Times Live ingawa Ginimbi anatambuliwa kuwa alikuwa ni mtu aliyerkuwa na uraibu wa kununua magari.

Magari haya ni ya kifahari na alinunua mfano aina tofauti za BMW, Jaguar na Lexus.

Genius Ginimbi showcase im cars

 

(Visited 7 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here