Home Makini Tech Vitu Unavyopaswa Kutofanya kwenye Simu

Vitu Unavyopaswa Kutofanya kwenye Simu

Je ni vitu gani ambavyo unatakiwa kutofanya kwenye simu yako kwa usalama na utunzaji wa simu yako? Tunatumia wakati mwingi sana kutumia simu janja zetu. Na tunapenda na kutamani kuziweka salama kadri tunavyokua tunazitumia. Lakini bila kukusudia tunafanya makosa kadhaa madogo ambayo hatupaswi kamwe kufanya na simu janja zetu.

Ingawa huwa hatuyaoni makosa haya madogo. Kwa ajili ya kuonyesha baadhi ya makosa haya, tumeunda orodha ya vitu ambavyo haupaswi kamwe kufanya na simu janja yako.

 

1- Usipakue programu / Apps kutoka vyanzo visivyojulikana

google playstore Kutofanya kwenye Simu
Kila uwezavyo tumia app ya Google PlayStore kupata apps zako muhimu

Wakati mwingine tunapakua programu yoyote kutoka kwa wavuti badala ya PlayStore. ambayo sio nzuri hata kidogo, kwa sababu programu hizi zinaweza kuwa na virusi au programu hasidi ambazo zinaweza kuiba habari yako nyeti. kwa hivyo twapendekeza kila wakati upakue programu kutoka Play Store kwa sababu tayari ina mamilioni ya programu, na hauitaji kupakua kutoka vyanzo visivyojulikana.

Soma maujanja mbalimbali yanayohusu utumiaji wa simu au kompyuta

2- Usiue Programu/ Apps ambazo umetumia hivi karibuni

Watumiaji wengi wa smartphone/ simu janja huua programu ambazo walikua wanazitumia hivi karibuni. Wanafikiri itaboresha utendaji au ufanisi wa simu zao. Je inaboresha utendaji wa simu janja? Hapana! Ila hupunguza utendaji wa simu janja zetu.

Wakati wowote tunapotumi app yoyote na kuhama, hua bado inajiendesha, ili wakati wowote tunapotaka tena kufungua app hiyo basi ifunguke kwa uharaka, inasaidia prosesa /processor ya simu kufungua app hiyo kwa haraka sana kwa sababu tayari imefunguliwa na kuhifadhiwa kwenye mfumo wa kumbumbu (cache memory).

Lakini unapoua / kuzima app baada ya kuitumia basi prosesa itabidi ifanye kazi zaidi kufungua tena programu hiyo tangu mwanzo, kitu ambacho kinaathiri utendaji wa simu yako.

3- Usitumie programu au apps za kusafisha simu

Daima tunataka kuhifadhi zaidi na zaidi, ndiyo sababu tunafuta programu au picha zisizo za lazima kutoka kwa simu yetu kudumisha uhifadhi. Lakini wakati mwingine tunapakua programu za kutusaidia kusafisha simu yetu ambayo hatupaswi kufanya hivyo.

Kusafisha mfumo wa kumbukumbu za ziada (cache memory) sio jambo zuri. App za kusafisha nafasi za ujazo katika simu yako zinaweza futa hadi data muhimu kwa programu/ app ambazo huwa unazitumia mara kwa mara, hili litafanya apps hizi zipate shida kufanya kazi tena utakapozingua – zitaanza upya, au ubaya zaidi itabidi apps hizo zidownload/kushusha data ambazo tayari ulikuwa nazo mwanzo.

4- Kutokuanzisha tena Simu janja yako (Not Restarting)

zima simu
Kuzima simu mara moja au mbili kwa wiki husaidia sana kuifanya simu yako kuwa na ufanisi mzuri

 

INAYOHUSIANA  Ndani ya siku 40 Samsung wauza Galaxy A milioni 2!

Hua tunatumia simu zetu mchana na usiku, na mara zote huwa tuwa tunatumia simu janja kwa muda mrefu bila kuzizima. Hiyo sio nzuri kwa simu janja yako, angalau unapaswa kuanzisha tena simu janja yako mara moja au mbili kwa wiki ili kuipatia programu endeshaji yako mwanzo mpya.

5- Usitumie simu yako wakati wa kuchaji

Usitumie simu yako wakati unachaji kwa sababu simu yako inaweza ikapata joto kali zaidi ukilinganisha na kama haitumika, hili linaweza kusababisha simu ichaji polepole na pia itaathiri maisha ya betri. Shida kubwa wakati mwingine ni kwamba matatizo ya simu kulipuka huwa uhusisha simu kupata joto kali, kwa hivyo epuka kutumia simu wakati wa kuchaji.

6- Kutokusasisha simu yako (Not Updating)

Shida moja ambayo watumiaji wengi wa simu janja hufanya ni pamoja na kutokusasisha simu zao. Sasisho zinafaa sana kwa usalama wa smartphone yako kwa sababu mara zote programu endeshaji ya simu yako huangalia kama simu yako ina mapungufu ya kiusalama katika toleo la mwanzo na hivyo hujaribu kuboresha usalama wa simu yako kwa kupitia masasisho ambayo yanafanyika kila baada ya muda fulani.

sasisho la simu
Kusasisha simu yako mara kwa mara inapohitajika itasaidia kuboresha ufanisi wa simu yako

 

INAYOHUSIANA  Viettel Imetangaza Nafasi za Ajira Kibao

Ikiwa walipata shida yoyote katika toleo la mwazo, kampuni zinatatua shida hiyo kwa kushinikiza sasisho, na pia, zinaongeza huduma mpya. Kwa hivyo kila wakati pendelea kusasisha simu yako utakapokua unapata taarifa za sasisho jipya kwani sasisho hili linaweza kuja na mambo mapya, au kuboresha mengine kama simu kukaa muda mrefu zaidi na chaji n.k.

7- Usitumie WiFi ya Umma

Wakati wowote tunapoona wifi ya umma tunachangamka na kutaka kuunganishwa na wifi hiyo, lakini hautambui ya kuwa ikiwa umeunganishwa na wifi ya umma basi nafasi ni kwamba simu yako sio salama. Simu yako inaweza kudukuliwa kwa urahisi sana. Kwa sababu kudukua simu ya mtu ikiwa ameunganishwa na WIFI ambayo ni ya umma ni rahisi zaidi.

Kama unataka kutumia huduma za kibenki au huduma zingine ambazo ni za kibinafsi sana basi epuka kuzifanya ukiwa unatumia huduma ya intaneti ya WIFI ambayo ni ya umma.

INAYOHUSIANA  Fairphone 2: Dondosha Simu Hii Kadri Unavyoweza! #Uchambuzi

Kwa hivyo ikiwa unahitaji haraka kutumia wifi ya umma basi unaweza kutumia VPN nzuri yoyote ili kuepuka kudukuliwa.

Je ni jambo gani katika haya umelikubali sana kwako kama ushauri kutoka kwetu? Je una cha kuongezea ambacho tumekisahau? Tutafurahi kusikia kutoka kwako.

(Visited 5 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here