Home Makini Newz Maafisa wa usalama wa uchaguzi wapinga madai ya wizi ya Trump

Maafisa wa usalama wa uchaguzi wapinga madai ya wizi ya Trump

 

Maafisa wa uchaguzi nchini Marekani wamesema kuwa kura za mwaka huu zilikuwa “mojawapo ya kura zilizolindwa zaidi katika historia ya Marekani “, na kupinga madai ya wizi wa kura.yaliyotolewa na Rais Donald Trump.

“Hakuna ushahidi kwamba mfumo wowote wa kupigia kura ulifutwa au kupotea kwa kura, kubadilishwa kwa kura, au ulifanyiwa mizengwe yoyote ile,” kamati ilitangaza.

Walizungumza baada ya Bw Trump kudai bila ushahidi kwamba kura zake milioni 2.7 zilikuwa “zimefutwa”.

Bado hajakubali kushindwa na rais mteule, Mdemocrat Joe Biden.

Matokeo ya uchaguzi wa tarehe 3 Novemba yalibashiriwa na karibu televisheni zote za Marekani TV mwishoni mwa juma lililopita.

Ubashiri wa BBC sasa kwamba Biden ameshinda Arizona, uliongeza ushindi wake kwa kura 11 wajumbe-ameshinda sasa 290, huku Trump akiwa na 217.nzisha upinzani wa kisheria taratibu dhidi ya makadirio ya kura katika majimbo muhimuna kutioa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa katika uchaguzi.

Wakati huo huo, China hatimaye imetoa pongezi zake kwa Bw Biden na mgombea mwenza Kamala Harris baada ya kimya cha siku kadhaa.

“Tunaheshimu chaguo la watu wa Marekani,” alisema msemaji wa izara ya mambo ya nje. Urusi imesema kuwa inataka kusubiri “matokeo rasmi”.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here