Home Makini Newz Ifahamu nchi inayoongoza kwa watumiaji wengi wa baiskeli

Ifahamu nchi inayoongoza kwa watumiaji wengi wa baiskeli

Usafiri wa baiskeli ya magurudumu Mawili uliundwa kwa kwa Mara ya kwanza na mjerumani Baron Karl von Drais aliyekuwa mfanyakazi wa serikalini, mnamo mwaka 1817 karne ya 19 C.

 

Uholanzi ndio nchi inyoongoza duniani kwa kuwa na watumiaji wa baiskeli Wengi zaidi.

 

Jumla ya idadi ya raia kitika sensa ni milioni 16,652,000 lakini kuna wamiliki na watumiji wa usafiri wa baiskeli zaidi ya milioni 16,500,000.

 

Sababu kuu iliyofanya waholanzi Wengi kutumia baiskeli ni baada ya ongezeko Vifo na ajali za barabarani hasa kwa watoto waishio maeneo ya mijini.

 

Vifo na ajali nyingi zilisababishwa na ongezeko la watumiaji Wengi wa vyombo vya moto kama Gari na pikipiki ktk miaka ya 1960s.

 

Sababu nyingine ya kutumia usafiri wa baiskeli kwa Wengi ni kuwa kama sehemu mojawapo ya kufanya mazoezi kwa mtumiaji husika.

 

Hali hii ilisabanisha wanaharakati wa haki za kibinadamu kukemea na kuhamasisha matuzi ya baiskeli zaidi kwa maeneo ya mijini kuliko vyombo vya moto kwani baiskeli ni salama zaidi na sio adui wa mazingira.

 

Kampeni hii ilifaulu na kufanya uholanzi kuwa nchi yenye waindesha baiskeli kuliko taifa lolote duniani kote na kupewa jina la utani la Netherlands ( Country of cyclists) “Taifa la waendesha baiskeli”

 

Nchi nyingine zenye watumiaji Wengi wa baiskeli badala ya uholanzi ni

 

· Denmark,

 

· Ujerumani

 

· Sweden,uswizi,

 

· Norway,

 

· Ubeligiji,

 

· Finland,China,T

 

· hailand,

 

· Indonesia).

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here