Home Makini Tech Programu Endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya simu Disemba...

Programu Endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya simu Disemba hii

Huawei wamekuwa kazini kwa miezi kadhaa wakitengeneza programu endeshaji ya ziada dhidi ya Android. Na sasa ni rasmi programu endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya kutumika kwenye simu kufikia Disemba mwaka huu.

Huawei wamesema toleo la kiwango cha beta litakuwa tayari kwa watengenezaji simu za mkononi (beta ni kiwango cha ubora unaoweza kutumika bila kuleta shida).

INAYOHUSIANA  Fahamu Internet.org Huduma ya Intaneti ya Bure Kutoka Facebook na Tigo

 

Rais wa masuala ya teknolojia katika upande wa Huawei unaohusika na biashara za bidhaa amesema kufikia Januari au Februari mwakani tayari tutegemee kuona simu zinazotumia programu endeshaji hiyo.

 Harmony OS itakuwa tayari
Inategemewa programu endeshi ya Harmony OS itakuwa tayari kwa makampuni ya utengenezaji simu pamoja na watengeneza apps kufikia Disemba 2020

 

Ingawa mabadiliko ya kiongozi wa serikali ya Marekani kutoka kwa Bwana Trump, kwenda kwa Rais aliyeshinda uchaguzi kwa sasa Bwana Joe Buden yanaweza kuleta mabadiliko flani katika katazo la kibiashara dhidi ya Huawei lakini Huawei bado hawategemei mabadiliko makubwa sana.

INAYOHUSIANA  Simu janja: Zifahamu Oppo A9 na A9x

Programu endeshi ya Harmony OS inategemea kuweza kuleta ushindani dhidi ya programu endeshaji ya Android. Huawei iliwalazimu kuja programu endeshaji yao ili kujiokoa kutoka kwenye vikwazo vya Marekani vinavyowabana kuweza kufanya kazi na Google, ambao ndio wamiliki na walezi wa programu endeshaji ya Android.

Je una mtazamo gani na maendeleo haya kutoka Huawei? Je unadhani watafanikiwa?

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here