Home Makini Tech Ujumbe mfupi wa WhatsApp unaweza kufutika baada ya siku saba

Ujumbe mfupi wa WhatsApp unaweza kufutika baada ya siku saba

WhatsApp disappearing messages

WhatsApp imeanzisha chaguo la kuwezesha ujumbe kujifuta baada ya siku saba kwa mtumiaji na kwa yule anayetuma.

Programu hiyo inayomilikiwa na Facebook-,ambayo ina watumiaji bilioni moja duniani kote, imesema mfumo huo utasaidia kuweka mawasiliano kuwa ya siri au binafsi.

Lakini watumiaji bado wataweza ‘ screenshot ‘ au kusambaza ujumbe wowote, picha au videos ambazo wanataka kuzihifadhi.

Mfumo huo utaanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Novemba.

Katika blogu, kampuni hiyo imesema ujumbe utawekewa siku ya mwisho kuepo baada ya siku saba ili kuwapa watu haueni ya mawasiliano ambayo si ya kudumu.

, huku kutasalia na kiashiria kuwa uliwalisiliana jambo gani”.

Mwezi Aprili 2019, Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg alifanya abadiliko kadhaa katika mitandao yake ya kijamii ili kuweka usiri wa mawasiliano zaidi.

Miongoni mwa mapendekezo ni namna ya kushirikishana maudhui , ikiwa ni pamoja na kupoteza ujumbe mfupi.

Kampuni hiyo ina tumaini kuunganisha majukwaa yake yote kuanzia WhatsApp, Instagram na Facebook Messenger kufanana.

Snapchat, imetoa msukumo kwa uwepo wa chaguo la ujumbe kupotea baada ya muda.

“Ikumbukwe kuwa suala hili lilikuwa lije kwa WhatsApp, muda mrefu sana na ilikuwa imezinduliwa mwaka 2017t.”

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here