Home Makini Newz Shirika la umma la Kiislamu lafungwa Ufaransa

Shirika la umma la Kiislamu lafungwa Ufaransa

Shirika la umma la Kiislamu la Baraka City, limeripotiwa kufungwa kufuatia uamuzi wa baraza la mawaziri nchini Ufaransa

Wazir wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin, alitangaza taarifa hizo za kufungwa kwa shirika hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya uamuzi kutolewa na baraza la mawaziri.

Darmanin alidai kuwa shirika la Baraka City limekuwa likihusika na uchochezi wa chuki na uadui kwa itikadi kali za Kiislamu , na kuunga mkono harakati na mashambulizi ya kigaidi.

Mnamo tarehe 14 Oktoba, mwanzilishi wa shirika la Baraka City Idriss Sihamedi alivamiwa nyumbani kwake na baadaye akaachiliwa huru siku iliyofuatia.

Na mnamo tarehe 16 Oktoba, mwalimu mmoja shule Samuel Paty katika eneo la Conflans-Sainte-Honorine lililoko karibu na Paris, aliuawa baada ya kuonyesha picha za katuni ya Nabii Muhammed.

Baada ya mauaji ya Paty, uvamizi wa mashirika ya Kiislamu uliongezeka ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Darmanin, alitoa tangazo tarehe 19 Oktoba kuhusu uamuzi wa kufunga mashirika ya umma ya Kiislamu kama vile CCIF, Baraka City pamoja na misikiti mingi.

(Visited 3 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here