Home Makini Newz Marekani yajaribu kuzuia uteuzi wa Mwafrika kuongoza shirika la biashara duniani WTO

Marekani yajaribu kuzuia uteuzi wa Mwafrika kuongoza shirika la biashara duniani WTO

Bi Okonjo – Iweala ana umri wa miaka 66 na ni raia wa kwanza mwanamke kutoka Nigeria aliyewahi kuwa waziri wa fedha na waziroi waziri wa kigeni

Uteuzi wa Waziri wa zamani wa biashara wa Nigeria kuongoza Shirika la Biashara Duniani (WTO) umekumbwa na utata baada ya Marekani kupinga hatua hiyo.

Siku ya Jumatano, kamati ya uteuzi ya WTO ilipendekeza wanachama 164 wamteue Ngozi Okonjo-Iweala.

Atakuwa mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza kuongoza WTO.

Lakini Marekani, ambayo imekuwa ikikosoa jinsi WTO inavyoshughulikia biashara ya kimataifa, inamtaka mwanamke mwingine Yoo Myung-hee, kutoka Korea Kusini ikisema huenda akabadilisha shirika hilo.

Lakini mchakato huo wa uteuzi wa miezi minne wa kumtafuta Mkurugenzi mkuu wa WTO umegonga mwamba baada ya Washington kusema itaendelea kumuunga mkono waziri wa biashara wa Korea Kusini.

Katika taarifa iliyokosoa WTO, ofisi ya mwakilishi wa biashara ya Marekani, ambayo humshauri Rais Donald Trump kuhusu sera za biashara, ilisema shirika hilo “lazima liongozwe na mtu wa kisawa sawa aliye na uwezo na tajiriba katika nyanja hiyo”.

Bi Yoo alikuwa “amejinadi” kama mtaalamu wa masuala ya biashara aliye na “ujuzi wote muhimu unaohitajika kuongoza shirika hilo”, taarifa hiyo ilisema.

Iliongeza: “Huu ni wakati mgumu sana kwa WTO NA biashara ya kimataifa . Hakujakuwa na majadiliano kuhusu masuala ya ushuru kwa miaka 25, mfumo wa kusuluhisha mizozo umesambaratika, na wanachama wachache sana hutimiza majukumu yao ya uwazi. WTO inahitaji mageuzi makubwa .”

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here