Home Michezo Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.10.2020: Kabak, Rice, Wilshere, Romero, Pochettino, McGurk,...

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.10.2020: Kabak, Rice, Wilshere, Romero, Pochettino, McGurk, White

Ozan Kabak

Liverpool imeanza mazungumza na Schalk kuhusu uhamisho wa mwaka mpya wa kitita cha karibu pauni milioni 20 kwa ajili ya mlinzi Ozan Kabak, 20, baada ya jeraha la muda mrefu la Virgil van Dijk. (Sunday Mirror).

aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal na england Jack wilshere, 28 anapendelea uhamisho wa kujiunga na ligi kuu ya kandanda Marekani MLS huku akutafuta klabu mpya baada ya kuondoka West Ham. (Sunday Mirror)

Mlinda mlango wa Manchester United,Muajentina Sergio Romelo anapanga mazungumzo na anataka kuondoka Old Trafford. Sergio, 33 ana matumaini kuwa makubaliano yatafikiwa kusitishwa mkataba wake baada ya kubaini kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameachwa kwenye kikosi cha United.(Star on Sunday)

Jack wilshere, 28 anapendelea uhamisho wa kujiunga na ligi kuu ya kandanda Marekani MLS

Leeds inataka kujaribu tena kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Wigan Sean McGurk , 17, baada ya ofa kukataliwa wakati wa dirisha la usajili lililopita. (Sun)

Kocha wa Brighton Graham Potter ametupilia mbali tetesi na kuhusisha na uhamisho wa mchezaji wa ulinzi Ben White, 23, kuelekea Liverpool kuwa ”kelele za kandanda”. (Sunday Mirror)

Mlinda mlango wa Manchester United,Muajentina Sergio Romelo anataka kuondoka Manchester

Mchezaji huyo wa zamani wa nafasi ya ulinzi ameiambia BBC kuwa White anaweza kufuata nyayo zake kwa kuhamia Liverpool , lakini hafikirii kama mabingwa hao wa ligi kuu watakamilisha mpango huo katika kipindi cha dirisha lijalo la usajili. (Argus)

Wolves, West Ham, Crystal Palace, Southampton na Newcastle wanamfuatilia nahodha wa Reading Liam Moore, 27. (Team Talk)

Ben White

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemhakikishia kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek,23, kuwa muda wake utakuja ndani ya Manchester United baada ya kuingia kwake kushindwa akuzaa matunda na kutoka 0-0 na Chelsea siku ya Jumamosi. (Manchester Evening News)

Solskjaer aliamua kuwa kikosi cha Manchester United kinapaswa kuwa pamoja katika hoteli ya Lowry kabla ya mechi ya Jumamosi, kwa mara ya kwanza tangu ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Manchester City mwezi Machi. (Star on Sunday)

Real Madrid imewasiliana na kocha wa zamani wa Tottenham na Southampton Mauricio Pochettino kuhusu uwezekano wa kupata mbadala wa Zinedine Zidane. (El Transistor)

Mauricio Pochettino

Kocha wa Liverpool Hurgen Klopp amesema kumuuza mshambuliaji wa England Rhian Brewster, 20 , kwa Sheffield United ”lilikuwa jambo gumu”. (Sunday Experss)

Beki wa kushoto wa Southampton Ryan Bertrand,31, ameunga mkono kampeni ya ligi ya primia ya ‘hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi’ baada ya kubainisha unyanyasaji alioupitia akuwa mtoto. (Sunday Mirror)

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here