Home Makini Newz Vurugu Nigeria: Jinsi maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yalivyobadilisha Nigeria

Vurugu Nigeria: Jinsi maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yalivyobadilisha Nigeria

Protesters at Lekki toll gate

Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi nchini Nigeria umebuni vuguvugu ambalo linaonekana kutikisa viongozi walio madarakani, lakini ni nini kitakachofuata baada ya msukosuko huo wa zaidi ya wiki mbili? Ufuatao ni uchambuzi wa Mhariri wa BBC Hausa Aliyu Tanko.

Mchanganyiko wa maandamano ya barabarani na kapeni katika mitandao ya kijamii imewapatia vijana wa Nigeria sauti kuvunja utamaduni wa nchi wa kujistahi.

Kadri Hashtag ya #EndSARS ilivyopata umaarufu mitandaoni, ndivyo ukaidi wa raia wa Nigeria ulivyoshika kasi.

Hatua ya kuharibiwa kwa makazi oba ama makao ya kiongozi wa kitamaduni mjini Lagos ilikuwa ishara ya mhemko huo.

Vijana waliburuza kiti chake cha enzi, wakapora mali zake na kuogelea kwenye dimbwi lake.

Maelezo ya video,Vurugu Nigeria: Mahushuda wa mauaji Nigeria wadai ‘polisi waliwapiga risasi’

Kile kilichoanza kama maandamano dhidi ya kikosi maalum cha polisi wa kukabiliana na wizi wa mabavu (Sars) kimegeuka kuwa nafasi ya vijana kuelezea kutoridhishwa kwao na watu waliopewa dhamana ya kuongoza Nigeria kwa miongo kadhaa, sasa wanataka mageuzi.

Rais wa zamani wa Olusegun Obasanjo mwaka 2017 alionya kuwa “wanakalia bomu ambalo linakaribia kulipuka” linapokuja suala la vijana.

Tamko lake lilikuwa kuhusu bara zima la Afrika lakini linashabihiana na hali ilivyo Nigeria, nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu (Milioni 200) Afrika, zaidi ya asilimia 60 wakiwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 24.

Idadi kubwa ya wale ambao wametimiza umri wakufanya kazi hawana ajira rasmi huku kukiwa na nafasi finyu ya kubata elimu bora. Mapema mwaka huu takwimu za serikali zilionyesha kwamba asilimia 40% ya Wanigeria wanaishi katika hali ya umasikini.

Haya sio maandamano ya kawaida

Lakini wale walio madarakani mwanzoni hawakuelewa kinachoendelea wakati huu, mwanaharakati na mwandishi Gimba Kakanda aliambia BBC.

Maandamano ya “#EndSARS awali yalichukuliwa kama njia moja ya uhuni wa vijana ambao utafifia ukipuuzwa,” alisema.

“Mtazamo huo wa viongozi wa kisiasa, wakutojali ndio umechangia kuimarika kwa vuguvugu la kupigania mageuzi ambalo limewaacha wote vinywa wazi.”

Swali ni je harakati hizo sasa zinaelekea wapi?

Ufanisi wa maandamano yaliyolazimisha serikali kutekeleza- kwa mfano ahadi ya kuvunga kikosi cha Sars na kufanyia mageuzi idara ya polisi – imewapatia ujasiri vijana wa Nigeria na sasa wanaamini wanaweza kuleta mabadiliko.

Siku chache baada ya kuanza kwamaandamano hayo, wanaharakati waliweza kubuni mkakati wa kushughulikia hali ya dharura. Pia walitoa huduma za kisheria kwa wale wanaohitaji na hata kuanzisha kituo cha redio.

Mikakati hiyo ilifadhiliwa kupitia michango ya kifedha ya pamoja ambayo imeonesha mfano wa jinsi Wanigeria wanaweza kupata huduma bora bila kutegemea wanasiasa ambao husaidia kwa maslahi yao ya kibinafsi badala ya jinsi wanavyoweza kuboresha nchi.

Lakini pia kumeshuhudiwa ghasia ambazo zimetia doa mkakati huo.

Lagos ilikumbwa na visa vya wizi na uporaji na Jumatano na Alhamisi
Maelezo ya picha,Lagos ilikumbwa na visa vya wizi na uporaji na Jumatano na Alhamisi

Wakati maandamano yaliyopangwa na vuguvugu la #EndSARS yalikuwa ya amani, kuna baadhi ya vijana ambao walitumia maandamano hayo kufanya vitendo vya uhalifu.

Walivunja maduka, kupora mabohari na kulenga biashara za wanasiasa mashuhuri.

Japo malengo ya makundi hayo mawili yalikuwa tofauti, wote walikuwa na ajenda moja: chuki dhidi ya wale walio husika.

Huenda ikawa vigumu kwao kufikia lengo la kupigania mageuzi ikiwa. Visa vya uvunjaji sheria vinavyoshuhudiwa huenda vikaathiri jitihada zavuguvugu hilo kufika maeneo mengine ya nchi kwasabau baadhi ya watu huenda wakaona vigumu kukaa meza moja na watu walio na “tabia inayotiliwa shaka”.

‘Buhari alikosa hoja

Mamlaka kwa upande wake unafahamu fika kwamba umasikini na hali ngumu ya maisha ni tishio kwa usalama wa kitaifa, mwanaharakati activist Bw. Kakanda alisema.

“Serikali imegundua kuwa haiwezi kupuuza tena malalmiko ya raia kama ilivyokuwa ikifanya awali,” aliongeza.

Lakini inaendelea kukosea hatua katika juhudi za kukabiliana na hali ilivyo.

Hotuba ya Rais Muhammadu Buhari kwa taifa siku ya Alhamisi “haikuwa na mashiko”, kwa mujibu wa mwanablogu na mchambuzi wa masuala ya kijamii Japheth Omojuwa.

Bw. Buhari alitoa wito wa kukomeshwa kwa maandamano ili kutoa nafasi kwa majadiliano, lakini “atakumbukwa kwa kuwatishia Wanigeria kwasababu ya kuomba serikali kuzingatia haki”.

Waandamanaji wa End Sars
Maelezo ya picha,Waandamanaji sasa wanatakiwa kufuatilia hatua zilizopigwa katika mageuzi ya polisi, mchambuzi anasema

Hata hivyo Bw. Omojuwa anaamini kuwa vugu vugu la #EndSARS linaweza kufikia lengo lake.

Wanachotakiwa kufanya ni kuwa na maono na wala sio kupata nyadhifa za kisiasa, badala yake anawaomba wahusika kuhakikisha mamlaka inazingatia ahadi ya mageuzi na kuhakikisha polisi wanaokiuka sheri awanachukuliwa hatua.

(Visited 5 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here