Home Makini Newz Rais wa Uturuki alaani uvamizi wa Msikiti wa Mevlana uliotekelezwa na polisi...

Rais wa Uturuki alaani uvamizi wa Msikiti wa Mevlana uliotekelezwa na polisi wa Berlin nchini Ujerumani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amekemea uvamizi wa msikiti wa Mevlana uliotekelezwa na polisi katika mji mkuu wa Berlin nchini Ujerumani.

 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Erdoğan alisema,

‘‘Ninakemea vikali operesheni ya msikiti wa Mevlana iliyoendeshwa na polisi mjini Berlin bila kujali uhuru wa kiimani na kudhihirisha ubaguzi, chuki na uadui wa wazi dhidi ya Uislamu.’’ Erdoğan pia alitoa pole kwa jamii nzima ya msikiti wa Mevlana.

‘‘Sisi kama Uturuki, hatuwezi kuruhusu ukiukaji wa haki za kiimani katika maeneo matakatifu ya ibada kwa kisingizio cha aina yoyote.’’

Erdoğn aliongezea kusema kuwa wataendeleza mapambano dhidi ubaguzi wa rangi, unyanyasaji wa wageni na uadui kwa Waislamu popote pale na kwa njia zozote zinazostahili.

‘‘Ulaya ambayo imekuwa ikikuza misingi ya kuzuia ukiukaji wa demokrasia, haki za kibinadamu na uhuru wa watu kwa miaka mingi, kwa bahati mbaya leo hii imekuwa na miundo tofauti katika kupambana na masuala hayo.’’

Katika  mji wa Berlin, kumekuwa na madai ya ukosefu wa uadilifu kwenye suala la msaada wa kifedha kwa wafanyabiashara wadogo walioathirika kwa janga la covid-19, na sehemu 4 za biashara zilivamiwa pamoja na msikiti huo.

Kitendo cha maafisa 150 wa polisi kuvamia msikiti wa Mevlana nyakati za asubuhi siku ya Jumatano na kuingia na viatu vilivyochafua mazulia na sehemu za ibada wakati wa sala, kiliibua hisia kali.

(Visited 1 times, 1 visits today)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here